| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
“Tuko pamoja na nyinyi”: Mkuu wa WHO aelekea DRC huku maambukizi yakifika zaidi ya 1,000
Tedros anasema nchi hiyo imefanikiwa kukabiliana na Ebola mara 16, atoa wito kwa watu kuungana kusaidia kwa haraka
“Tuko pamoja na nyinyi”: Mkuu wa WHO aelekea DRC huku maambukizi yakifika zaidi ya 1,000
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom anaelekea DRC huku maambukizi ya Ebola yakizidi 1,000. / Reuters

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema siku ya Alhamisi kuwa anaelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku kukiwa na mlipuko mwingine wa Ebola.

“Ebola imerudi,” Ghebreyesus alisema katika ujumbe kwenye mtandao wa X. “Nitakuwepo DRC na wahudumu wa WHO, washirika na wahudumu wengine wa afya ambao wamekuwa wakikabiliana na hali muda wote.”

Akiahidi kufanya kila kitu “ndani ya uwezo wake” kusaidia kudhibiti mlipuko huo hatari, aliongeza katika ujumbe mrefu kwa watu wa DRC: “Nataka niwe pamoja na nyinyi kipindi hiki. Na nataka nyinyi mjue kuwa hamko peke yenu.”

Amesema mkoa wa Ituri “umeathirika zaidi” kwa mlipuko huo na kwamba serikali ya DRC imekuwa ikiongoza juhudi za kukabiliana na hali.

Wamefanikiwa mara kumi na sita

Mkuu wa WHO amesisistiza kuwa DRC imefanikiwa kukabiliana na milipuko ya Ebola hapo awali.

“Mara kumi na sita, nchi hii imefanikiwa kudhibiti Ebola. Huu mlipuko wa 17 pia itafanikiwa ,” Tedros amesema. “Lakini lazima tuchukue hatua kwa pamoja sasa.”

Idadi ya maambukizi ya Ebola imepita zaidi ya 1,000 huku yakiongezeka mikoa ya mashariki, kulingana na taarifa ya tathmini ya hali iliotolewa siku ya Jumatano na Wizara ya Afya.

CHANZO:TRT Afrika and agencies