Serikali ya Mali imekataa kuzungumza na makundi ya kigaidi, waziri wa mambo ya nje amesema, baada ya magaidi na wanaotaka kujitenga kufanya mashambulizi kote nchini.
Mashambulizi hayo ya magaidi na jamii ya Tuareg inayotaka kujitenga Aprili 25 na 26 yalilenga miji muhimu na kumuua waziri wa ulinzi wa nchi hiyo.
"Serikali ya Mali haina mpango wa kufanya majadiliano na makundi ya kigaidi yenye silaha ambayo yanahusika na matukio mabaya waliopitia watu wetu kwa miaka mingi," Waziri wa Mambo ya Nje Abdoulaye Diop amesema, wakati alipokutana na mabalozi siku ya Alhamisi.
Nchi hiyo ya Afrika Magharibi imekuwa ikikabiliwa na vurugu kwa zaidi ya muongo mmoja na mashambulizi ya mwezi uliopita yalikuwa kumbukumbu ya vurugu zilizoikumba Mali 2012.
Mashambulizi katika miji
Chini ya muungano ulioundwa mwaka mmoja uliopita, jamii ya Watuareg wanaotaka kujitenga waliungana na kundi la kigaidi la JNIM kufanya mashambulizi ya hivi karibuni.
Waziri wa Ulinzi Sadio Camara aliuawa katika shambulizi hilo eneo la Kati, mji wenye kambi za kijeshi karibu na mji mkuu. Rais Assimi Goita sasa amechukua majukumu hayo ya ulinzi kwa muda.
Tangu 2012, Mali imekabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa usalama lililosababishwa na vurugu za makundi ya kigaidi na wanaotaka kujitenga. Vurugu hizi zilisababisha mzozo wa kisiasa, na hadi kuwepo kwa matukio mawili ya mapinduzi ya kijeshi 2020 na 2021.


















