| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Umoja wa Mataifa unasema msaada kwa watu wa Somalia huenda ukasitishwa mwezi Juni
Somalia inakabiliwa na matatizo kadhaa, ikiwemo mashambulizi ya kigaidi ya kundi la Al-Shabaab dhidi ya serikali kuu.
Umoja wa Mataifa unasema msaada kwa watu wa Somalia huenda ukasitishwa mwezi Juni
Afisa wa WFP nchini Somalia kutathmini athari za Mashariki ya Kati kwa tatizo la njaa / Reuters

Somalia inakabiliwa na tatizo la utapiamlo na inahitaji msaada zaidi wa haraka kuepuka baa, Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa limesema siku ya Ijumaa, likionya kuwa huenda likalazimika kusitisha misaada kwa watu kuanzia Julai iwapo hawatopata ufadhili zaidi.

Ukosefu wa misimu kadhaa ya mvua, ambayo imesababisha mimea na mifugo kudhoofika, na mapigano yanayoendelea na ukosefu wa usalama imesababisha watu wa Somalia kuwa katika viwango vya hatari vya njaa wakati misaada ya kutoka nje ikipungua kutokana na vita dhidi ya Iran, WFP imesema.

Watu milioni 6 nchini Somalia, karibu mtu mmoja kati ya watatu, wanakabiliwa na njaa mbaya, ilhali watoto milioni 1.9 wakiwa na utapiamlo kwa sasa, kulingana na WFP.

"Somalia inakabiliwa na utapiamlo mbaya na sehemu yenye utapiamlo hatari duniani," Matthew Hollingworth, mkurugenzi msaidizi wa WFP, aliwaambia waandishi wa habari mjini Geneva. Akizungumza kwa njia ya video kutoka mjini Rome.

WFP pamoja na mashirika ya misaada kwa watu pia wanakabiliwa na uhaba wa ufadhili wa kuokoa maisha ya watu, huku vyakula vya tayari vikichelewa kwa hadi siku 40, kutokana na kutatizwa kwa mifumo ya usambazaji kulikosababishwa na vita Mashariki ya Kati, Hollingworth amesema.

CHANZO:TRT Afrika Swahili