Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, amefika mjini Roma, Vatican kwa ajili ya kikao na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo XIV.
Mazungumzo hayo yanakuja wakati kukiwa na mvutano wa wazi kati ya Ikulu ya Vatican na Makao Makuu ya Kanisa Katoliki duniani.
Ziara hiyo, pia inakuja baada ya Rais Donald Trump wa Marekani, kukosoa waziwazi msimamo wa Papa Leo XIV, kuhusu vita.
ZILIZOPENDEKEZWA
Hata hivyo, Rubio ambaye ni muumini wa dhehebu la Kikatoliki, amepuuzia madai ya uhasama kati ya pande hizo mbili, kabla ya ziara hiyo ambayo pia itahusisha mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin.
Ziara hiyo, imeratibiwa na Ikulu ya Marekani, kulingana na Kardinali Parolin.
CHANZO:AFP

















