| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
DRC yafuzu kucheza Kombe la Dunia baada ya kusubiri kwa miaka 52
Timu hiyo sasa inajiunga na Ureno, Colombia na Uzbekistan katika kundi moja kuwania kombe hilo la dunia.
DRC yafuzu kucheza Kombe la Dunia baada ya kusubiri kwa miaka 52
Mchezo huo wa kukata na shoka, ulifanyika Jumanne usiku, katika dimba la Estadio Guadalajara nchini Mexico./Picha:Wengine
tokea masaa 2

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imefuzu kushiriki michuano ya Kombe la Dunia, itakayoanza siku 71 zijazo.

Bao la dakika ya 100 lililofungwa na beki wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza, Axel Tuanzebe dhidi ya Jamaica, liliwahakikishia Les Léopards, nafasi ya kushiriki michuano hiyo mikubwa duniani, inayoandaliwa kwa pamoja na Marekani, Mexico na Canada.

Mchezo huo wa kukata na shoka, ulifanyika Jumanne usiku, katika dimba la  Estadio Guadalajara nchini Mexico.

Inakuwa mara ya pili kwa DRC kukata tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia, baada ya kushiriki kwa mara ya kwanza mwaka 1974, wakati huo ikijulikana kama Zaire.

Pia, ilikuwa ni nchi ya kwanza kusini mwa jangwa la sahara, kufuzu kwa michuano hiyo, kwa wakati huo.

DRC ilifika hatua hii baada ya kuifunga Nigeria katika mchuano muhimu kati ya timu za Afrika na baadaye kufuzu katika fainali na kukutana na timu kutoka bara lingine, ili kutafuta nafasi hiyo ya kufuzu.

Timu hiyo sasa inajiunga na Ureno, Colombia na  Uzbekistan katika kundi moja kuwania kombe hilo la dunia.

CHANZO:TRT Afrika Swahili