Wizara ya Ulinzi ya Marekani, maarufu kama Pentagon, inakabiliwa na uhaba mkubwa wa fedha, kutokana na taifa hilo kuendelea kupigana na Iran.
Likiwanukuu maofisa wa Marekani siku ya Jumanne, jarida la The Washington Post limesema kuwa uhaba huo wa fedha, umelilazimu jeshi la Marekani kupunguza mazoezi na matengenezo ya vifaa vya kijeshi.
Inadaiwa kuwa, kushindwa kufikiwa kwa sitisho la kumaliza vita dhidi ya Iran, kutaongeza gharama zaidi kwa wizara hiyo.
Hayo yanajiri wakati Ikulu ya White House nchini Marekani, ikiomba kuidhinishiwa Dola bilioni 67, kama mfuko wa dharura, japo haijapitishwa bado na bunge la Congress.
CHANZO:AA












