| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Mzee wa miaka 90 aweka rekodi ya kukwea kilele cha Mlima Kilimanjaro
Katika tukio hilo Dkt. Ulene alikata keki akiwa amezungukwa na waongoza watalii, wapagazi, na wapandaji wenzake huku wakimpongeza kwa ujasiri, wakimtakia afya njema na kumpongeza kwa azma yake ya kutimiza ndoto hiyo katika umri wa miaka 90.
Mzee wa miaka 90 aweka rekodi ya kukwea kilele cha Mlima Kilimanjaro
Akizungumza mara baada ya kupokelewa, Dkt. Ulene alitoa shukrani kwa uongozi wa KINAPA, waongoza watalii na wapagazi kwa ushirikiano na huduma bora al

Mmarekani Art Ulene, ameandika historia mpya baada ya kufanikiwa kufika katika Kilele cha Uhuru, Mlima Kilimanjaro, na kuvunja rekodi ya kuwa mtu mwenye umri mkubwa zaidi kufikia kilele hicho, Julai 13, 2026.

Dkt. Ulene, mwenye umri wa miaka 90, alikwea kilele cha Uhuru kwenye Mlima wa Kilimanjaro na kukata keki juu ya kilele hicho, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa.

Katika tukio hilo Dkt. Ulene alikata keki akiwa amezungukwa na waongoza watalii, wapagazi, na wapandaji wenzake huku wakimpongeza kwa ujasiri, wakimtakia afya njema na kumpongeza kwa azma yake ya kutimiza ndoto hiyo katika umri wa miaka 90.

Mara baada ya kuweka rekodi hiyo, Dkt. Ulene ambaye ni daktari mstaafu, alipokelewa na maofisa kutoka Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro (KINAPA), Julai 16, 2026, na kupongezwa kwa kutambua mchango wake katika kutangaza utalii na uhifadhi wa Mlima Kilimanjaro mara baada ya kuvunja na kuandika rekodi mpya ya mtu mwenye umri mkubwa kufika katika kilele cha mlima mrefu barani Afrika akiwa na umri huo.

Mapokezi hayo yaliambatana kwa vifijo na nderemo  vilivyogubikwa kwa nyimbo na shamrashamra kutoka kwa wahifadhi, waongoza watalii kutoka kampuni ya World Wide Trekking na wapagazi walioambatana na mgeni huyo tangu mwanzo hadi mwisho wa safari yake ndani Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro.

Akizungumza mara baada ya kupokelewa, Dkt. Ulene alitoa shukrani kwa uongozi wa KINAPA, waongoza watalii na wapagazi kwa ushirikiano na huduma bora alizopatiwa katika kipindi chote cha safari yake.

Kulingana na Dkt. Ulene, kupanda Mlima Kilimanjaro akiwa na umri wa miaka 90 ni ushahidi kwamba ndoto zinaweza kutimia bila kujali umri endapo mtu atajipanga vizuri na kufuata ushauri wa wataalamu.

"Nitarejea nyumbani nikiwa na ujumbe mmoja kuwa Tanzania ni nchi salama, yenye watu wakarimu na vivutio vya kipekee. Nitawahamasisha Wamarekani na watu kutoka mataifa mengine kuja kushuhudia uzuri wa Mlima Kilimanjaro na hifadhi nyingine za taifa," alisema Dkt. Ulene.

Kwa upande wake, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Angela Nyaki alieleza kuwa  KINAPA inaamini kuwa tukio hili litavutia watalii wengi zaidi kutoka Marekani na kote duniani, jambo ambalo litaongeza mapato ya serikali na kusaidia kuboresha miundombinu ya hifadhi.

CHANZO:TRT Afrika Swahili