| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Uturuki inaweka historia kwa kusafirisha treni ya kwanza iliyotengenezwa nchini humo kwenda Afrika
Treni hiyo iliyopelekwa Tanzania ilitengenezwa na kampuni ya Uturuki ya vifaa vya reli, Turasas, anasema Waziri wa Uchukuzi wa Uturuki.
Uturuki inaweka historia kwa kusafirisha treni ya kwanza iliyotengenezwa nchini humo kwenda Afrika
Lokomotiv ya kwanza ya Uturuki iliyotengenezwa nchini humo yasafirishwa kwenda Afrika / TRTWorld / TRT World

Treni ya kwanza ya kuvuta mabehewa inayotumia mfumo wa dizeli na umeme na kutengenezwa nchini Uturuki imesafirishwa kwenda Afrika, jambo linaloashiria hatua muhimu katika sekta ya reli ya nchi hiyo.

Waziri wa Uchukuzi, Abdulkadir Uraloglu, alisema katika taarifa yake siku ya Jumatatu kuwa treni hiyo ya aina ya DE 10000 ilitengenezwa na kampuni ya Uturuki ya utengenezaji wa vifaa vya reli, Turasas.

"Tulituma treni yetu ya kuvuta mabehewa aina ya DE 10000 kwenda Tanzania , Treni yetu, ambayo ni matokeo ya uhandisi wa ndani," alisema.

Uraloglu alisema Treni hiyo ilisafirishwa kwenda Tanzania tarehe 29 Julai na itawasili katika Bandari ya Dar es Salaam.

Uraloglu aliongeza kuwa treni hiyo ina injini ya dizeli ya kwanza kabisa kutengenezwa nchini Uturuki yenye nguvu ya zaidi ya farasi 1,000, iliyoundwa kwa ushirikiano kati ya Turasas na Taasisi ya Utafiti wa Kisayansi na Teknolojia ya Uturuki (Tubitak).

"Ujuzi wa kihandisi na uwezo wa usanifu uliopatikana wakati wa utengenezaji wa injini hiyo uliinua kiwango cha uwezo wa kiteknolojia wa Uturuki katika mifumo ya nishati, kwani injini hiyo ni bidhaa muhimu kimkakati inayokidhi mahitaji ya sekta mbalimbali, hasa sekta ya reli," aliongeza.

CHANZO:َAA
Soma zaidi
Waziri wa zamani wa ulinzi wa Israel Yaalon amshtumu Netanyahu kwa uchokozi dhidi ya Uturuki
Uturuki itaendelea kuwa chanzo cha matumaini kwa Gaza na dunia: Erdogan
Kenya, Uturuki kushirikiana zaidi katika biashara, uwekezaji na ulinzi
Uturuki yachapisha rasmi sheria ya mchakato wa 'Uturuki Isiyo na Ugaidi'
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki afanya mazungumzo na mawaziri wenzake wa Qatar na Syria
Chombo cha Uturuki cha Marlin chaimarisha uwezo wa kutegesha mabomu baharini
Uwanja wa ndege wa Istanbul waweka rekodi mpya ya ndege na abiria
'Matatizo ya usalama' katika mpaka wa Uturuki na Syria yametoweka: Balozi wa Uturuki
Miaka 25 ya Chama cha AK na kuimarika kwa Uturuki kama mdau muhimu katika kanda na ulimwenguni
Uturuki yataka Tunisia kumuachia kiongozi wa chama cha Ennahda
Austria na Uturuki: Hatua nyingine ya ushirikiano
Uturuki imekamata washukiwa 30 katika operesheni dhidi ya shirika la uhalifu la Alihan Kuris
Erdogan aapa kuipigania dola ya Kipalestina
Rais Erdogan wa Uturuki kukutana na Abbas jijini Ankara kujadili hali ya Palestina
Katika picha: Vivutio mbalimbali vya Uturuki vyang’aa mwanga kushangilia mkataba wa Ulinzi wa Mecca
Rais Erdogan wa Uturuki akutana Kansela Stocker wa Austria
Ndege ya Bayraktar TB2 ya Uturuki yasaidia kudhibiti moto wa nyika nchini Albania
Makubaliano ya Makka ni ya ulinzi wa pamoja lakini hayalengi shabaha au adui yeyote: Waziri Fidan
Uturuki yaadhimisha kumbukumbu ya miaka 59 ya ASEAN na kuahidi kuimarisha ushirikiano wa kikanda.
Uturuki yakanusha madai kuwa Mkataba wa Ulinzi wa Makkah unakinzana na Kifungu cha 5 cha NATO