Wakati Chama cha AK kikiadhimisha miaka 25 Agosti 14, Uturuki inaangazia robo karne iliopita kama kipindi ambacho taifa liliimarika katika ngazi za kimataifa.
Kiliingia madarakani muda mfupi baada ya kuundwa kwake, chama hicho kimeleta mabadiliko makubwa nchini Uturuki, ndani ya nchi na kimataifa.
Serikali ya Chama cha AK ilichukua uongozi kwa kuondoa urasimu katika usimamizi wa jeshi, ikihimiza kutambua umuhimu wa utamaduni na jamii, kuimarisha uchumi na uhusiano kati ya watu na taifa.
Ikiwa tayari imejiimarisha katika masuala ya ndani ya nchi, chama hicho kikachukua nafasi ya kuangazia kuhusu kuunda na kutekeleza sera ya mambo ya nje – ile ambayo iliimarisha ukuaji wa nafasi ya Uturuki katika kanda na ulimwenguni.
Katika miaka yake ya awali, serikali ya Chama cha AK iliangazia kuimarisha uchumi na nafasi yake kimataifa, ikiwa na malengo ya uwanachama wa Umoja wa Ulaya na uhusiano bora na majirani zake.
Iliangazia Mashariki ya Kati, mataifa ya Balkan, Afrika, Caucasus, Asia ya Kati, na maeneo mengine ya mbali, yote kwa lengo la kuimarisha uchumi na uwezo wake katika kanda.
Suala la msingi katika mabadiliko haya ni kuimarisha uwezo wa kiuchumi, kupanua mtandao wa kidiplomasia, na mifumo ya usalama katika sera ya mambo ya nje.
Kulingana na takwimu za Benki ya Dunia, GDP ya Uturuki iliongezeka kutoka Dola bilioni 236 hadi Dola trilioni 1.6 mwaka 2025.
Serikali ya Chama cha AK ilipanga kuendeleza uhusiano wa Uturuki bila kuvunja uhusiano na mataifa ya Magharibi.
Mwanzo wa majadiliano ya EU mwaka 2005 ilikuwa ni suala la kuangazia mataifa ya Magharibi, wakati EU ikitaka kupunguza uhasama na majirani zake, kufungua milango kwa Afrika, uhusiano mzuri wa kiuchumi na nchi za Ghuba, na kuimarisha ushirikiano wa kitaasisi na Asia ya Kati.
Huku ikiungwa mkono na umma na kuwa na ushawishi kimataifa, Rais Recep Tayyip Erdogan na washirika wake waliondoa uwezo wa jeshi katika masuala ya raia kwa kubadilisha baadhi ya vipengele vya katiba na sheria.
Kipindi cha muongo wa pili cha uongozi wake, Chama cha AK kilibidi kukabiliana na vuguvugu la kubadilisha utawala nchi za Kiarabu katika mataifa ya Mashariki ya Kati, vurugu nchini Syria, taharuki Mashariki mwa Mediterania, jaribio la mapinduzi la Julai 15, chuki za mataifa ya Magharibi kwa uhuru wa Uturuki, mvutano kati ya Urusi na Ukraine, na marufuku ya Qatar.
Baada ya mchakato huu, Uturuki ikawa inaangazia mfumo wa usalama na mchakato wa kufanya maamuzi huru.
Uhuru huu wa kimkakati ulitoa muelekeo kwa sera ya mambo ya nje ya Uturuki katika kipindi cha miaka kumi na tano iliopita. Mabadiliko ya katiba ya 2011, ambayo yalimaliza ubabe wa jeshi, iliwezesha utekelezaji wa kuendesha sera za ulinzi kwa uwazi zaidi.
Kuimarika kwa Uturuki kimkakati
Uongozi wa kiraia wa Chama cha AK umeimarisha uhusiano wa NATO wakati ikianzisha uhusiano na mataifa mengine, ikiwemo Urusi, Asia ya Kati, Ghuba, Asia, na Afrika.
Kwa uhuru huu, Uturuki imeimarisha uwezo wake wa kijeshi.
Huku uzalishaji wa ndani wa sekta ya ulinzi ukiwa asilimia mbili 2002, leo hii uzalishaji huo umeongezeka zaidi ya asilimia 80 na bado unaimarika, mafanikio muhimu.
Teknolojia za Uturuki za UAV, meli za kivita, magari yenye silaha, mifumo ya makombora, na uwezo wa kutumia teknolojia katika vita imesaidia uchumi wa Uturuki na kuwa sehemu ya sera yake ya mambo ya nje ilioimarisha uhusiano na Pakistan, Ukraine, mataifa ya Ghuba, Afrika, na Asia ya Kati.
UAV ya Bayraktar na awamu ya 5 ya ndege za kivita za KAAN zimekuwa muhimu duniani.
Kwa matokeo ya mafanikio haya, Mauzo ya vifaa vya ulinzi na vya anga vya Uturuki nje ya nchi yameongezeka kutoka Dola milioni 248 milioni mwaka 2002 hadi Dola bilioni 10.05 2025.
Maendeleo katika sekta ya ulinzi yamewezesha Uturuki kukamilisha operesheni zake za kijeshi kwa uhuru kabisa, lakini pia inawekeza zaidi katika utafiti na maendeleo ili kuziba pengo lililopo.
Uwezo wa kijeshi wa Uturuki umedhihirika nchini Libya kwa kutibua mapinduzi ya kijeshi huko 2020. Usaidizi wa jeshi la Uturuki ulisaidia Azerbaijan kukomboa maeneo yake yaliyokaliwa mwaka huo huo.
Katika kipindi cha karne mbili zilizopita, Uturuki imeongeza uwepo wake wa kijeshi na ushirikiano na mataifa mengi, ikiwemo Somalia, Qatar, Libya, Pakistan, na Azerbaijan.
Agosti 7, ilianzisha muungano wa ulinzi wa mataifa matatu pamoja na Pakistan, nchi pekee ya Kiislamu yenye nyuklia, na Saudi Arabia, moja ya wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani.
Mataifa mengine ya Kiarabu pia yanatarajiwa kujiunga na muungano huo, kuanzisha enzi za ushirikiano wa usalama katika kanda na uimarishaji wa mifumo ya kuhimiza amani.
Serikali ya Chama cha AK iliimarisha shughuli za kidiplomasia za Uturuki kote duniani.
Kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje, Mitandao ya kibalozi ya Uturuki ilifika 262, kufanya kuwa moja ya mitandao mikubwa ya ubalozi duniani.
Kwa mfano, kulikuwa na balozi 12 pekee barani Afrika 2002, idadi hiyo iliongezeka hadi 44 mwaka 2026.
Kiwango cha biashara, kati ya Uturuki na Afrika kiliongezeka kutoka karibu Dola bilioni 3 hadi Dola bilioni 36.6 wakati huo, na Shirika la Turkish Airlines sasa linasafiri katika miji 64 ya Afrika.
Uturuki iliimarisha uhusiano thabiti wa kiuchumi na kidiplomasia na mataifa ya Balkan na Asia ya Kati.
Mataifa ya Balkan, Uturuki ikaanzisha Jukwaa la Amani la Balkan 2025 kuzuia kuzuka tena kwa mapigano ya zamani na kuimarisha ushirikiano kwa masuala ya usalama mipakani, nishati na uchukuzi.
Katika Asia ya Kati, Uturuki iliongoza mabadiliko ya Shirika la Mataifa yanayozungumza Kituruki 2021, kuimarisha uhusiano wa kitaasisi wa Uturuki na kanda.
Wakati huo huo, Uturuki ikaimarisha uhusiano wake na mataifa muhimu ya Kiarabu kama vile Saudi Arabia na Misri baada ya kipindi cha hali tete wakati wa harakati za mabadiliko ya uongozi katika mataifa ya Kiarabu, huku Syria ikifaidika zaidi.
Nafasi ya Uturuki katika upatanishi na mzozo wa kidiplomasia ulisababisha dunia kuangazia suala hilo pia.
Katika miaka ya nyuma, Uturuki ilikuwa mpatanishi kati ya Bosnia na Serbia, Syria na Israel, Iran na Marekani, Urusi na Ukraine, Afghanistan na Pakistan, na Ethiopia na Somalia, pamoja na makundi ya Iraq.
Hivi karibuni, ilikuwa mpatanishi wa mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi wakati wa vita vya Urusi na Ukraine 2022. Hili liliepusha ukame na ugumu wa maisha katika baadhi ya maeneo duniani, kudhihrisha uwezo wa Uturuki wa diplomasia.
Diplomasia ya misaada pia ni sehemu muhimu ya sera ya mambo ya nje ya Uturuki.
Taasisi kama vile TIKA, Yunus Emre, Ufadhili wa masomo wa Uturuki, Wakfu wa Maarif, AFAD, Shirika la Hilali Nyekundu la Uturuki, na Shirika la Turkish Airlines zimeendeleza uhusiano wa kijamii wa Uturuki kwa kupitia njia mbalimbali.
Kulingana na OECD, Uturuki ilitoa msaada wa maendeleo wa karibu Dola bilioni 7.3 mwaka 2024; Dola bilioni 6.1 ulikuwa msaada kwa watu.
TIKA ina ofisi zake za uratibu katika nchi 61, 22 zikiwa barani Afrika.
Shule zinazofadhiliwa na Maarif zinatoa mafunzo kwa maelfu ya wanafunzi nje ya Uturuki,na baadhi yao hupata ufadhili wa masomo wa kusoma Uturuki.
Zaidi ya hayo, uchumi, nishati na uunganishaji ni sehemu muhimu ya uwezo wa kidiplomasia wa Uturuki.
Mauzo ya nje ya nchi ya Uturuki yaliongezeka kutoka karibu Dola bilioni 36 mwaka 2002 hadi Dola bilioni 273 mwaka 2025, ikiwa ni mafanikio makubwa.
Mabomba ya mafuta kama vile TANAP, TurkStream, Baku-Tbilisi-Ceyhan, Kerkük-Yumurtalik, na Baku-Tbilisi-Kars yameimarisha kuunganisha nafasi ya Uturuki kati ya Ulaya, Caucasus, Mashariki ya Kati, na Asia ya Kati.
Zaidi ya Mlango Bahari wa Hormuz
Kufungwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz wakati wa vita vya Iran na Marekani kuliongeza umuhimu wa mataifa ya Kiarabu kuunganishwa na Uturuki, kama ilivyokuwa kwa miradi ya barabara, reli, na mabomba ya mafuta.
Mataifa yote ya Ghuba na Iraq yanataka njia kupitia Magharibi mwa Uturuki, ambayo inaridhishwa na mpango huu mpya wa ushirikiano.
Kupatikana kwa gesi asilia kwenye Bahari Nyeusi imekuwa faida kubwa kwa Uturuki tangu 2020.
Hivi karibuni, sera ya mambo ya nje ya Uturuki imekuwa muhimu zaidi katika mashirika ya kimataifa ili kutoa muelekeo kwa agenda za kikanda na dunia.
Nafasi yake muhimu katika majukwaa kama G20, NATO, Shirika la Mataifa ya Kiislamu, D-8, na Shirika la Mataifa yanayozungumza Kituruki; kuimarika kwa Jukwaa la Diplomasia la Antalya na kuwa jukwaa la kimataifa; na juhudi za upatanishi ndani ya Umoja wa Mataifa na OSCE ni mifano ya mtindo huu.
Hata hivyo, uwezo wa kuelekeza agenda hautoi hakikisho la kupatikana tija, huku Uturuki ikiangazaia maafikiano kwa kuwahusisha wadau wote wakati mmoja, hata wale ambao wanakuwa wanatofauatiana.
Mwisho, kuimarika kwa ushawishi wa Uturuki kimataifa wakati wa uongozi wa robo karne wa Chama cha AK ikumbukwe ni kutokana na uwezo wa juhudi za kidiplomasia za muelekeo wa faida kwa wote, ukisaidiwa na uchumi thabiti, sekta ya ulinzi, biashara, misaada kwa watu, nishati, uchukuzi, na ushirikiano na kimkakati.
Ilijiweka katika hatari Libya na Karabakh wakati ilikuwa sahihi kufanya hivyo.
Kutilia umuhimu taasisi za kimataifa, sheria, na ushirikiano, Uturuki inazingatia umuhimu katika masuala ya amani kwenye kanda na duniani.
Kutoka mataifa ya Balkan hadi Afrika, kutoka Bahari Nyeusi hadi Asia ya Kati na Mashariki ya Kati, Uturuki ni mdau muhimu wa kutambulika katika maeneo kadhaa.
Uzoefu wa kitaasisi, mitandao ya kidiplomasia, na uwezo wa teknolojia katika kipindi cha miaka 25 iliopita imeandaa Uturuki kwa nafasi muhimu zaidi duniani.
Kuendelea kwake kutategemea kuimarishwa kwa ustahmilivu wa uchumi na kupunguza utegemezi katika nishati pamoja na kuimarisha teknolojia.




















