| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Zimbabwe yatangaza hali ya dharura kufuatia ajali ya kivuko huku idadi ya waliofariki ikifika 44
Idara ya kukabiliana na Majanga ya Zimbabwe (CPU) siku ya Jumatano ilisema kuwa kivuko hicho kilikuwa na abiria wasiopungua 114.
Zimbabwe yatangaza hali ya dharura kufuatia ajali ya kivuko huku idadi ya waliofariki ikifika 44
Shirika la habari la taifa ZBC limeonesha video za mashua za uokoaji zikielekea eneo la ajali katika ziwa hilo.

Idadi ya waliofariki katika ajali ya kivuko nchini Zimbabwe imeongezeka hadi 44 huku Rais Emmerson Mnangagwa akitangaza hali ya dharura kwa janga hilo siku ya Jumatano.

Kivuko hicho kilizama katika Ziwa Kariba siku ya Jumanne baada ya mawimbi makali na kupindukia, kulingana na polisi.

Kivuko hicho kilitengenezwa kwa ajili ya abiria 90, lakini zaidi ya abiria 120 huenda walikuwemo wakati huo kikivuka ziwa lililo karibu na mpaka na Zambia, polisi walisema katika taarifa.

Kati ya abiria hao 12 walikuwa watoto, kulingana na taarifa.

Waliosajiliwa kwenye tiketi

“Polisi nchini Zimbabwe wameeleza kuwa idadi ya waliofariki kwenye ajali ya kivuko Kariba sasa ni 44,” iliongeza.

Idara ya CPU ya Zimbabwe ilisema siku ya Jumatano kuwa kivuko hicho kilikuwa na abiria 114 na wahudumu watano kulingana na waliosajiliwa.

Idadi isiojulikana ya watoto inaaminika pia walikuwa miongoni mwa abiria, jambo linalofanya iwe vigumu kujuwa idadi kamili ya waliokuwemo ndani. Mamlaka zinasema kivuko hicho kilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 90 pekee.

CHANZO:TRT Afrika Swahili