| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Uturuki yataka Tunisia kumuachia kiongozi wa chama cha Ennahda
Spika wa Bunge la Uturuki, Numan Kurtulmus, amesema Rached Ghannouchi anahitaji matibabu kufuatia umri wake na hali yake ya afya.
Uturuki yataka Tunisia kumuachia kiongozi wa chama cha Ennahda
"Kwa kuzingatia umri wake na matatizo ya kiafya aliyonayo, uzito wa hali ya Ghannouchi haupaswi kupuuzwa," amesema Kurtulmus. / / Anadolu Agency

Spika wa Bunge la Uturuki, Numan Kurtulmus, siku ya Alhamisi ametoa wito kwa kiongozi wa Harakati ya Ennahda na Spika wa zamani wa Bunge la Tunisia, Rached Ghannouchi, ambaye yuko gerezani, kupewa matibabu na kuachiwa kwa kuzingatiwa utu na ubinadamu.

Kurtulmus amesema kupitia NSosyal, mtandao wa kijamii wa Uturuki, kwamba anafuatilia kwa karibu hali ya Ghannouchi, ambaye amemtaja kuwa “miongoni mwa watu mashuhuri katika mapambano ya amani, demokrasia na mshikamano.”

Amongeza kuwa Ghannouchi amesitisha kugoma kula na kutumia dawa, baada ya kuombwa kufanya hivyo na madaktari wanaofuatilia hali yake.

“Kwa kuzingatia umri wake mkubwa na matatizo ya kiafya aliyonayo, uzito wa hali ya Ghannouchi haupaswi kupuuzwa,” alisema Kurtulmus.

Amemtaja Ghannouchi kuwa mtu aliyejitolea maisha yake kwa “mustakabali wa watu wa Tunisia, uhuru, haki na demokrasia,” akisema licha ya shinikizo, na kuishi uhamishoni na kufungwa, hakuachana na “maadili aliyoyaamini na mapambano yake ya kidemokrasia.”

Kurtulmus amesema Ghannouchi amepata kutambuliwa kwa kiwango kikubwa nchini Tunisia na kimataifa kutokana na “msimamo wake wa kidemokrasia wakati wa kipindi cha mpito, msingi wake imara wa kielimu na mawazo yake.”

“Kwa kuakisi uhusiano wa kina wa kindugu uliopo kati ya watu wa Uturuki na Tunisia, namuombea afya njema na natumaini kwamba atarejea katika hali nzuri ya kiafya haraka iwezekanavyo,” alisema.

“Jambo tunalolitamani zaidi ni kwamba apewe kikamilifu msaada wa matibabu unaohitajika, apewe mazingira ya haki na ya kibinadamu yanayohitajika kwa ajili ya kuheshimu utu wa binadamu, na aachiliwe.”

Kuzuiliwa kwa Ghannouchi

Ghannouchi, ambaye alikuwa Spika wa Bunge lililovunjwa na Rais Kais Saied, amekuwa gerezani tangu alipokamatwa Aprili 17, 2023.

Mahakama iliamuru azuiliwe katika kesi iliyohusiana na matamshi yaliyodaiwa kutolewa na yeye, akishtakiwa kwa “kuchochea dhidi ya usalama wa taifa.” Baadaye alihukumiwa kifungo chaa gerezani katika kesi kadhaa, lakini ameyakataa mashtaka hayo na kusema kuwa yana msukumo wa kisiasa.

CHANZO:Anadolu Agency
Soma zaidi
Erdogan akiwa UNGA: Akumbushia kuhusu taifa la Palestina na kuhimiza mabadiliko duniani
Emine Erdogan ahimiza kuachana na ‘utamaduni wa kutupa vitu’ na kuelekea kwenye matumizi endelevu
Uturuki inalenga kubadilisha ahadi za hali ya hewa kuwa vitendo katika COP31: Waziri wa Mazingira
Rais Erdogan asema uhusiano wa Uturuki, Marekani lazima 'uimarike zaidi', vikwazo viondolewe
Erdogan apigia upatu mageuzi ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Uhusiano wa Uturuki na Marekani unavuka mipaka ya kijeshi, asema Kilic
Ni masuala gani muhimu ambayo Erdogan wa Uturuki atawasilisha katika hotuba yake kwa UN?
Mkuu wa Intelijensia wa Uturuki kukuza ushirikiano na Libya
Rais Erdogan awasili New York kuhudhuria Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Rais wa Uturuki Erdogan kuzuru Marekani kwa ajili ya kikao cha 81 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Mchakato wa 'Uturuki Isiyo na Ugaidi' wakaribia hatua ya mwisho licha ya uchochezi: Rais Erdogan
Njia ya nne ya kurukia ndege uwanja wa Istanbul kukuza uchukuzi, asema Rais Erdogan
Uturuki yawakamata watu 175 wanaohusishwa na utapeli  mitandaoni unaohusiana na wamiliki wa Kiisrael
Hurkus-II ndege ya kwanza kutengenezwa Uturuki kukabidhiwa Jeshi la Anga ya nchi hiyo
Uturuki na mataifa mengine yalaani shambulizi la Houthi dhidi ya Mecca
Mkuu wa Intelijensia wa Uturuki aitembelea Afghanistan
Hali ya Mlango Bahari wa Hormuz irudi kama kawaida, asema Fidan
'Asante, Uturuki' — Wasomali wanasherehekea kuimarika kwa uhusiano na Ankara
Erdogan apongeza ongezeko la ufaulu nchini Uturuki
Uturuki: msamaha wa silaha wa Marekani kwa Utawala wa Kigiriki wa Cypriot unahatarisha uaminifu