| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Uhusiano wa Uturuki na Marekani unavuka mipaka ya kijeshi, asema Kilic
Jopo hilo liliandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki, pembezoni mwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, jijini New York.
Uhusiano wa Uturuki na Marekani unavuka mipaka ya kijeshi, asema Kilic
Jopo hilo liliandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki, pembezoni mwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, jijini New York.

Mshauri wa Rais wa mambo ya nje na usalama, Akif Cagatay Kilic amesema kuwa uhusiano kati ya Uturuki na Marekani unavuka mipaka ya kijeshi, huku NATO ikibakia kuwa, nguzo kuu ya uhusiano huo.

"Uhusiano tulionao ni tofauti na mahusiano mengine tuliyonayo na mataifa tofauti,” alieleza Kilic, siku ya Jumatatu, katika jopo maalumu jijini New York.

Jopo hilo liliandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki, pembezoni mwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, jijini New York.

Jopo hilo, lilihudhuriwa na Cagri Erhan, ambaye ni makamu mwenyekiti wa Baraza la Ulinzi wa Usalama na Mambo ya Nje, balozi wa zamani wa Marakeni nchini Uturuki, James Jeffrey, na balozi wa zamani wa Marekani nchini Azerbaijan Matthew Bryza.

"Nadhani NATO inabakia kuwa nguzo muhimu ya uhusiano wetu," alisema.

Wakati huo huo, Erhan alisisitizia umuhimu wa kihistoria wa uhusiano huo, akibainisha kuwa ulianzia wakati wa zama za himaya ya Ottoman.

Alitoa mfano wa namna Marekani ilivyoingia vitani wakati wa vita Kuu ya Kwanza ya Dunia bila kuishambulia dola ya Ottoman.

"Walitangaza vita dhidi ya Ujerumani na si dhidi ya dola ya Ottoman."

'Tunaishi dunia moja'

Kwa upande wake, Jeffrey aliangazia maslahi ya pamoja kati ya Uturuki na Marekani.

"Ninaweza kuzungumzia taasisi mbalimbali kama vile IMF, Benki ya Dunia, OECD na NATO, lakini ni zaidi ya taasisi,” alisema.

Kwa mujibu wa Jeffrey, Uturuki ina uwezo wa kuwa na ushawishi katika eneo lote la Mediterania na Ulaya.

"Tunashirikiana kwa kiasi kikubwa, hata tunapotofautiana,” alisema.

Wakati huo huo, tukio hilo liliambatana na maonesho ya picha, yaliyoandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki, katika eneo la kuingilia la ukumbi huo, kama ishara ya kuadhimisha miaka 100 ya ushirikiano kati ya Uturuki na Marekani.

 

 

CHANZO:Anadolu Agency