Hotuba ya Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan katika Mkutano Mkuu wa 81 wa Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne iliangazia masuala kadhaa kutoka kwa mauaji ya halaiki Gaza, mpango wa Israel wa upanuzi, vita vya Urusi na Ukraine, Bahari Nyeusi, Malngo-Bahari wa Hormuz na Caucasus ya Kusini.
Akisoma pamoja na hotuba yake kwa Umoja wa Mataifa ya 2025, makala yake ya Bloomberg na mikutano yake ya kidiplomasia jijini New York, hotuba ya 2026, hata hivyo, inadhihirisha mabadiliko makubwa ya sera ya mambo ya nje ya Uturuki.
Uturuki inaweka pamoja shutuma zake za matatizo hayo katika mfumo wa kimataifa ikuwa na mapendekezo ya namna matatizo hayo yanaweza kutatuliwa.
Jambo la uzito ambalo imeliendeleza kati ya 2025 na 2026 ni Palestina.
Hotuba ya Erdogan ya 2025 iliangazia Gaza, kushtumu vita vya mauaji ya halaiki vya Israel na msimamo wake katika kanda, kutambua taifa la Palestina na kuhamasisha jamii ya kimataifa.
Msimamo huo bado uko vile vile mwaka 2026, lakini agenda imekuwa pana zaidi ikiwemo kusisitiza kuhusu kusitishwa mapigano, kuingia hatua yake ya pili, ujenzi mpya wa Gaza, maendeleo katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, UNRWA na suluhu ya mataifa mawili.
Msisitizo wake kwa hospitali na His emphasis on hospitals and basic infrastructure in Gaza also fits within this wider framework.
Kwa hiyo suala la Palestina linaonesha kuondoka kwa hali ilivyo sasa hadi katika ujenzi upya na kupona majeraha kutoka kwa mauaji ya halaiki.
Mabadiliko zaidi ni kwa Erdogan kuukosoa Umoja wa Mataifa.
“Dunia ni kubwa kuliko mataifa matano” imekuwa moja ya hoja aliyoiwekea msisitizo, inayolenga tatizo la uwakilishaji katika Baraza la Usalama na upendeleo ya wanachama watano wa kudumu.
Mwaka 2026, muundo wa msingi uko nyuma ya ukosoaji huu. Makal ya Erdogan katika Bloomberg ni muhimu zaidi hapa.
Mapendekezo yako wazi: ondoa kura ya turufu, achana na kuongeza wigo wa wanachama zaidi wa kudumu, maliza mfumo wa wanachama wa kudumu na wanachama wa Baraza la Usalama wawe wanachaguliwa na Mkutano kwa muda maalum.
Hili linafanya ukosoaji wa Uturuki uwe zaidi ya uwezo wa wanachama watano wa kudumu.
Hoja hapa ni kuwa na uwezo mkubwa wenyewe wa kudumu. Jibu la Uturuki ni mfumo kwa misingi ya uchaguzi, mzunguko na uwajibikaji kwa jumla.
Katika ujumbe wa Erdogan wa 2026, upinzani unageuka na kuwa muundo wa kitaasisi.
Masuala ya kikanda
Mtindo huo huo unaonekana katika mfumo mwingine: suala la kikanda.
Katika mpango wa Rais, kanda zinazokabiliwa na matatizo zinatakiwa kutumia uwezo wake wa kisiasa na kidiplomasia vyema.
Akiashiria makubaliano ya Makkah – yaliyotiwa saini na Uturuki, Saudi Arabia na Pakistan kama mfumo wa kikanda – ni muhimu zaidi kwa muktadha huu.
Mfumo kama huo unaonekana kwa msisitizo wa“uongozi wa Libya na umilikaji,” kwa kuunga mkono majadiliano katika kanda kwenye nchi za Balkan na mchakato wa kutafuta yanayoibuka kutoka katika kanda kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz.
Hili halitakiwi kuonekana kama Uturuki kuachana na mfumo wa kiusalama wa Magharibi kwa mfumo mbadala.
Erdogan pia alisisitiza kuhusu umuhimu wa Uturuki kwa usalama wa Ulaya.
Kinachotokea kinaonekana kama mkakati wa kiusalama unaofungamana: uanachama wa NATO unaendelea, huku mifumo ya ulinzi katika kanda, ushirikiano wa mataifa na diplomasia ya upatanishi ikiendelezwa pamoja nayo.
Matatizo ya usalama kwa jirani za Uturuki yanaathiri moja moja Uturuki, kufanya uthabiti wa kanda kuwa msingi wa Uturuki kwa sera ya mambo ya kigeni na usalama .
Kwa sehemu kubwa mikutano ya New York inaakisi mfumo huu na masuala mengine: uunganishaji.
Kwa Erdogan, njia za barabara, biashara, nishati na uzalishaji wa pamoja siyo tu masuala ya kiuchumi, lakini ni nyenzo za usalama na uthabiti.
Ndiyo maana usafiri na biashara ni masuala yaliyojadiliwa pamoja na usalama katika mkutano wa na Waziri Mkuu Irakli Kobakhidze wa Georgia katika Jumba la Uturuki, na msisitizo wake kuhusu mpango wa ushirikiano wa Uturuki-Georgia-Azerbaijan.
Ukraine na zaidi
Moja ya mada muhimu ni uhusiano kati ya upatikanaji wa chakula na usalama katika Bahari Nyeusi.
Kwa mtazamo wa Uturuki, vita vya Urusi na Ukraine sasa ni zaidi ya diplomasia ya kusitisha mapigano.
Usalama wa meli za biashara katika Bahari Nyeusi, kufikishwa kwa nafasi katika soko la dunia bila pingamizi na kufungua njia za bahari zinazohusiana moja kwa moja na upatikanaji wa chakula duniani.
Mtazamo wa Uturuki unajulikana: badala ya kuangazia kutatua vita vyote kupitia makubaliano makubwa, inaangazia sehemu moja moja ambapo pande zote mbili zitakuwa zinakutana kimaslahi.
Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi wa 2022 ulikuwa mfano dhahiri: ulifanikiwa huku vita vikiendelea, kuruhusu nafaka ya Ukraine kufika katika masoko ya kimataifa na uliangaziwa na Uturuki kama mchango wake katika kusaidia upatikanaji wa chakula duniani.
Mwaka 2026, mbinu hiyo hiyo inatumika kwa mfumo mpana zaidi wa usalama wa baharini kwa kuzingatia meli za biashara, usalama wa baharini na upatikanaji wa chakula.
Hili linaashiria njia muafaka ya upatanishi ambayo Uturuki inapendelea: weka mifumo ya msingi wakati wa migogoro na tumia hiyo kuweka mazingira ya kuwa na makubaliano mapana ya kisiasa.
Uturuki inataka kuimarisha nafasi yake kitaasisi na namna ambayo mizozo inatatuliwa.
Agenda ya tabianchi pia inakwenda kwa mfumo huo huo.
Kuwepo kwa mkutano unaoangazia utekelezaji wa COP31, kusisitiza uwekezaji wa fedha na teknolojia kwa nchi zinazoendelea, na kuwaalika viongozi kuja Antalya wakiwa New York inaonesha namna gani ujumbe kutoka Umoja wa Mataifa unatiliwa mkazo kupitia diplomasia.
Palestina, Bahari Nyeusi, Libya, Caucasus ya Kusini, Mabadiliko ya Umoja wa Mataifa na upatikanaji wa chakula yanaweza kuonekana kama masuala tofauti.
Lakini hotuba ya Erdogan yameunganisha yote kwa mtazamo mmoja ambao pia unaendala na mada ya mwaka huu ya Umoja wa Mataifa ya kuimarisha imani.
Mwaka 2025, ujume wa Uturuki uliangazia migogoro inayoendelea, kueleza udhaifu wa mifumo ya kimataifa na kusisitiza kuhusu uwezo upatanishi wa Uturuki.
Msimamo huo bado upo 2026, lakini sasa unatilia mkazo na mapendekezo thabiti katika ngazo ya utekelezaji.
Masuala ya kikanda, uunganishaji, upatanishi halisi, kuzuia kwa pamoja, upatikanaji wa chakula na uwakilishaji mpana katika taasisi za kimataifa yanazidi kuwa sehemu sera hiyo hiyo ya mambo ya nje.
Hilo ndilo linalotofautisha hotuba ya Erdogan ya mwaka 2026. Upinzani na ukosoaji wa muda mrefu sasa unabadilishwa na kuwa mapendekezo thabiti.
Uturuki inataka kuimarisha nafasi yake kama mdau anayeweka mizania kati ya migogoro za kuwa mpatanishi.
Kuwa na usalama wa kikanda na mfumo wa uunganishaji, kuweka wazi njia za kimkakati za biashara, kuwa na nafasi muhimu katika masuala ya upatikanaji wa chakula duniani na kuwa na uwakilishi halisi katika taasisi za kimataifa inakuwa jambo la kutiliwa msisitizo ili kutimiza azma hiyo muhimu.



















