Mkuu wa Intelijensia wa Uturuki Ibrahim Kalin, amefanya mazungumzo na mwenzake wa Libya, Abdussalam Zubi, jijini Istanbul.
Kikao hicho cha siku ya Jumamosi, kinakuja wakati wa jitihada za kuzileta pamoja taasisi za kijeshi na za kisiasa za Libya.
Wawili hao, walijadiliana mambo mbalimbali ikiwemo ushirikiano wa mataifa hayo mawili, huku Zubi akiishukuru Uturuki kwa jitihada zake za kuiunganisha Libya, huku Kalin akisisitiza haja ya kuendelea kuisaidia Libya.
Uhusiano kati ya nchi hizo mbili, umezidi kuongezeka katika miaka ya hivi karibuni, hususani katika nyanja za kiusalama, biashara na usafiri wa majini.
Novemba 2019, nchi hizo zilisaini mkataba muhimu wa majini, ambao umeendelea kuwa sehemu muhimu ya uhusiano kati ya Libya na Uturuki.
Makubaliano hayo, pia yamewezesha kukua kwa uhusiano kati ya Uturuki na Libya.
Hali kadhalika, Uturuki imeendeleza juhudu za kuunganisha taasisi za Libya.
Mwezi Agosti, Kalin alisema kuwa Uturuki itaendelea na jitihada za kuzileta pamoja taasisi za Libya.
Kikao cha wawili hao, kinakuja wakati mataifa hayo yakilenga kuendelea kushirikiana.






















