Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amepongeza kiwango cha ufaulu cha Uturuki kwa mwaka 2025, akibainisha kuwa kiwango hicho katika masomo ya kusoma, kuandika na sayansi kimeongezeka kwa asilimia 50.
Akizungumza siku ya jumatatu wakati wa ufunguzi wa mwaka mpya wa masomo jijini Ankara, Erdogan alisema Uturuki, limekuwa taifa pekee kufanya hivyo kati ya nchi za OECD.
Kulingana na Erdogan, hakuna sababu za kudharau mafanikio hayo, huku akiwataka raia wa nchi hiyo kujisikia fahari kwa mafanikio hayo.
Kulingana na OECD, Uturuki imefanya vizuri kuliko mataifa mengine ya OECD, hususani katika masomo ya sayansi, kusoma na hisabati.
Nchi hiyo, imeshuhudia ongezeko hilo la ufaulu katika masomo hayo, ukilinganisha na kiwango cha ufaulu kwa mwaka 2022.
Utafiti huo, ulihusisha mataifa 91, ikipima uwezo wa wanafunzi wenye umri wa miaka 15, huku Uturuki ikishiriki toka mwaka 2003.



















