| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Algeria yasitisha uhusiano wake wa kidiplomasia na UAE
Hatua hii inaashiria kudorora kwa uhusiano kati ya nchi mbili za Kiarabu.
Algeria yasitisha uhusiano wake wa kidiplomasia na UAE
Algeria yavunja uhusiano wa kidiplomasia na Umoja wa Falme za Kiarabu

Algeria imetangaza kusitisha uhusiano wake wa kidiplomasia na Umoja wa Falme za Kiarabu, na kusema imetumia njia zote za kudumisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Uamuzi huo ulitangazwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria, kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Shirika la Habari la Algeria (APS).

"Algeria imeamua siku ya Alhamisi kusitisha uhusiano wake wa kidiplomasia na UAE baada ya kutumia njia zote za kudumisha uhusiano kati ya nchi mbili, kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje," imeandika APS.

Wizara haikutoa taarifa zaidi ya sababu ya kuchukua uamuzi huo.

Hatua hiyo inaonesha kuendelea kuzorota kwa mahusiano kati ya nchi hizo mbili za Kiarabu.