Raia wawili wa Misri waliokuwa wanafanya ibada ya Umrah wamefariki, na wengine 25 kujeruhiwa baada ya ajali ya basi karibu na mji wa Al-Jumum nchini Saudi Arabia maili 17 kutoka Makkah, Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri ilisema siku ya Jumapili.
Wizara inasema basi hilo, lililokuwa limebeba mahujaji 47 wa Misri, lilikuwa likisafiri kutoka mji wa Madina kuelekea Makkah wakati wa ajali hiyo Jumamosi jioni.
Watu 25 walipata ajali, ikiwemo saba waliolazwa katiba chumba cha wagonjwa mahututi, kulingana na taarifa.
Mahujaji waliobaki walitibiwa na kuruhusiwa kuondoka hospitali kabla ya kurudi tena katika hoteli zao mjini Makkah.
Mamlaka nchini Saudi Arabia hazikuzungumza mara moja chochote kuhusu ajali hiyo.
Umrah ni ibada isiyo lazima ya Waislamu ambayo ni hajj ndogo mjini Makkah inayojumuisha kutufu Kaaba.
AFRIKA
1 dk kusoma
Watu wawili wafariki, wengine 25 wajeruhiwa baada ya basi la mahujaji wa Misri kupata ajali Makkah
Mamlaka nchini Saudi Arabia hazikuzungumza mara moja chochote kuhusu ajali hiyo.

Soma zaidi


















