| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Erdogan ampongeza Meloni kwa kuwa Waziri Mkuu wa Italia aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anasema anatarajia kuwa ushirikiano na umoja kati ya Uturuki na Italia utaimarika zaidi.
Erdogan ampongeza Meloni kwa kuwa Waziri Mkuu wa Italia aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi
MAKTABA: Erdogan akipeana mikono na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni walipokutana villa Doria Pamphilj, jijini Roma, Aprili 29 2025.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amempongeza Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni baada ya kuwa Waziri Mkuu wa Italia kuwepo madarakani kwa muda mrefu zaidi.

"Nampongeza kwa dhati Bi. Giorgia Meloni, kwa kupata sifa ya kuwa waziri mkuu aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi nchini Italia,'" Erdogan alisema katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii siku ya Ijumaa.

Erdogan alisema ana imani kuwa uhusiano kati ya Uturuki na Italia utaimarika zaidi.

"Naamini kuwa tutaimarisha ushirikiano na umoja kati ya nchi zetu pamoja na Bi. Giorgia Meloni kila siku," alisema.

Siku ya Ijumaa Meloni rasmi alitimiza kuiongoza serikali kwa muda mrefu katika historia ya Jamhuri ya Italia, kulingana na shirika la habari la Italia ANSA. Alitimiza siku 1,413 ofisini tangu alipoingia madarakani Oktoba 22 2022, na kushinda serikali ya muhula wa pili ya Silvio Berlusconi, ambayo ilikuwepo kwa siku 1,412.

Meloni, ambaye pia amekuwa waziri mkuu aliyehudumu kwa muda mrefu kipindi ambacho si cha vita, aliandika ujumbe kwenye mtandao wa X, akitoa shukrani zake na kueleza kuhusu heshima ya jukumu hilo.

"Ni kweli kuwa nimeshkuru kwa hili na heshima kubwa ya jukumu hili. Kwa sababu usalama siyo jambo la kujisifia, lakini hali hiyo inatoa fursa kwa taifa kupanga, kuamua, kutimiza ahadi zake, na kuwa na heshima," alisema.

CHANZO:َAA