| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Uturuki kuongeza ushirikiano na Muungano wa Ushirikiano wa Shanghai: Rais Erdogan
Rais wa Uturuki anasema kuwa muungano huwo unaweza kuchangia katika amani, usalama wa njia za usafirishaji na usalama wa nishati, huku Uturuki ikimarisha ushirikiano wa karibu zaidi na kundi hilo.
Uturuki kuongeza ushirikiano na Muungano wa Ushirikiano wa Shanghai: Rais Erdogan
Erdogan alisema kuwa shirika hilo linaweza kuwa na mchango si tu katika kuhakikisha amani na utulivu, bali pia katika kuanzisha njia salama. / / Anadolu Agency

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema nchi yake inalenga kuimarisha zaidi ushirikiano na Muungano wa Ushirikiano wa Shanghai (SCO), akiitaja muungano huo kuwa ni “nyota inayochipukia”.

Rais Erdogan amesema Uturuki itajitahidi kuendeleza ushirikiano na Shirika la Ushirikiano la Shanghai katika nyanja zote.

“Tutaendelea kujitahidi kuendeleza ushirikiano wetu katika kila nyanja na Muungano wa Ushirikiano wa Shanghai, ambalo tunaiona kuwa nyota inayochipukia,” Erdogan amesema siku ya Jumanne katika mkutano wa SCO Plus mjini Bishkek, mji mkuu wa Kyrgyzstan.

Amesema Muungano wa Ushirikiano wa Shanghai, unaowakilisha watu Bilioni 3.5 na jumla ya pato la ndani la takribani Dola trilioni 35, ni sehemu muhimu isiyoweza kupuuzwa katika mfumo wa dunia wenye pande nyingi.

Erdogan amesema Uturuki inachukua nafasi ya kusaidia kutatua migogoro kupitia mazungumzo na diplomasia, na itaendelea na juhudi hizo kwa ajili ya amani na utulivu duniani.

Kwa mujibu wa Erdogan, muungano huwo unaweza kuwa na nafasi si tu katika kuhakikisha amani na utulivu, bali pia katika kuanzisha njia salama za usafirishaji na kuhakikisha usalama wa upatikanaji wa nishati.

Uturuki yataka ushirikiano mkubwa zaidi wa kikanda

Erdogan amesema Uturuki inalenga kuchangia katika juhudi za kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Alibainisha pia kuwa nchi hiyo itakuwa mwenyeji wa mkutano wa COP31 mjini Antalya tarehe 11–12 Novemba.

Amesema Uturuki inataka mpango wa njia ya ‘Middle Corridor’ unaopita katika Bahari ya Kaspian ulinganishwe na Mpango wa China wa Belt and Road, huku akisisitiza umuhimu mkubwa ambao Uturuki inaweka katika ushirikiano ndani ya Muungano wa Ushirikiano wa Shanghai.

Akizungumzia hali ya Gaza na Lebanon, Erdogan amesema watu 74,000 wameuawa kufuatia mashambulizi ya Israel, na akaonya kuwa eneo zima linabeba uzito wa kile alichokiita sera ya uchokozi.

Pia amesema Muungano wa Ulinzi wa Makkah, unaozingatia umiliki wa masuala ya kikanda na uwezo wa pamoja wa kuzuia vitisho, ungeweza kutoa mchango mkubwa katika kuleta amani na utulivu katika eneo hilo na duniani kwa ujumla.

CHANZO:Anadolu Agency