| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Erdogan, Putin wapongeza ushirikiano wa Uturuki na Urusi katika mkutano wa SCO
Viongozi hao waliangazia maendeleo kuhusu mradi wa Akkuyu na ushirikiano zaidi wa kiuchumi huku Uturuki na Urusi wakieleza nia ya kuimarisha miradi ya pamoja.
Erdogan, Putin wapongeza ushirikiano wa Uturuki na Urusi katika mkutano wa SCO
Marais Erdogan na Putin wamefanya mazungumzo pembeni mwa Mkutano wa Muungano wa Ushirikiano wa Shanghai jijini Bishkek Septemba 1, 2026. (AA)

Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan anasema kuwa uhusiano kati ya Uturuki na Urusi umefika katika hatua nzuri zaidi wakati alipokutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin nchini Kyrgyzstan.

Viongozi hao wawili walifanya mazungumzo siku ya Jumanne pembeni mwa Kongamano la Viongozi wa Nchi za Muungano wa Ushirikiano wa Shanghai (SCO) jijini Bishkek, huku Erdogan akisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa mataifa yao.

“Uhusiano wa Uturuki na Urusi kwa kweli umefika hatua ya juu kuliko wakati mwingine wowote,” Erdogan alisema.

Alisema mkutano huo ulikuwa fursa muhimu ya kuimarisha ushirikiano uliopo sasa na kuongeza miradi mingine.

Mradi wa Akkuyu umefika hatua ya mwisho

Erdogan alieleza kuwa Mtambo wa Umeme wa Nyuklia wa Akkuyu kama nguzo muhimu ya ushirikiano wa mataifa yao mawili, akisema mradi huo sasa umefika hatua ya mwisho.

“Kwa ufunguzi wa Mtambo wa Umeme wa Nyuklia wa Akkuyu, kwa mara nyingine tutachukua hatua ya kufungua mitambo mingine ya umeme,” alisema.

Wakati huo huo Putin, anasema ushirikiano wa kiuchumi kati ya Urusi na Uturuki bado ni wa hali ya juu, akipongeza ari ya Erdogan katika kuimarisha uhusiano wa mataifa hayo mawili.

Rais wa Urusi anasema nchi hizo mbili zinaendelea kutekeleza miradi ya pamoja, ikiwemo wa umeme wa Akkuyu, na kueleza imani kuwa sehemu ya kwanza itazinduliwa mwaka huu.

Mkutano huo ulisisitiza ushirikiano wa kiuchumi kati ya Uturuki na Urusi, huku suala la nishati likiwa moja ya maeneo ya msingi.

CHANZO:TRT World and Agencies