| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Cabo Verde yatangaza maombolezo ya kitaifa baada ya vifo vya watoto katika ajali ya basi
Wafanyakazi wa dharura walishughulika usiku kucha kuwaokoa waliokuwa wamekwama kwenye sehemu ya basi hilo
Cabo Verde yatangaza maombolezo ya kitaifa baada ya vifo vya watoto katika ajali ya basi
Watu saba walizikwa siku ya Jumapili . Picha/ Shirika la Habari la Cabo Verde

Serikali ya cabo Verde imetangaza siku mbili za maombolezo siku ya Jumapili baada ya watu 25, wengi wao wakiwa watoto na vijana kufariki, katika ajali ya basi.

Viongozi wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi walijumuika katika Maombi ya Jumapili kanisani katika kisiwa cha Fogo, ambapo kulikuwa na majeneza 18.

Maafisa wanasema basi lilitoka nje ya barabara na kuingia kwenye mtaro Jumamosi jioni.

Waziri Mkuu Francisco Carvalho ameiambia televisheni ya taifa TCV kuwa ametangaza siku mbili za maombolezo na kuahidi kuwa hatua zaidi zitachukuliwa.

Wakati huohuo, Rais Jose Maria Neves, anasema kuwa ataagiza kufanyika kwa uchunguzi kuhusu ajali hiyo.

Safari ya shule

Neves aliieleza ajali hiyo kama "masikitiko makubwa" na "yenye uchungu mkubwa kwa taifa.

"Natoa salamu zangu za rambirambi kwa familia, marafiki, kisiwa chote cha Fogo, na Cabo Verde kwa msiba huu," Mkuu wa Nchi alieleza alipowasili katika kisiwa cha Fogo," Neves alisema.

Mamlaka zimeripoti kuwa watu 25 wamefariki. 20 walifariki katika eneo la ajali, na watano walifariki katika Hospitali ya Kanda ya São Francisco de Assis, kulingana na takwimu rasmi zilizopatikana kufikia sasa.

Kati ya 14 waliojeruhiwa, watatu wako katika hali mbaya.

Serikali inasema itagharamia mazishi ya waliofariki kwenye ajali ya basi.

Watu saba walizikwa siku ya Jumapili.

CHANZO:TRT Afrika Swahili