Israel imeitaka Uingereza kufunga ubalozi wake mdogo katika Jerusalem Mashariki inayokaliwa na kwamba maafisa wanaofanya kazi hapo watafutiwa vibali vyao ndani ya siku 30, afisa mmoja wa Israel na vyanzo viwili vinavyofahamu kuhusu suala hilo vimesema.
Wajumbe wa Uingereza wanaofanya kazi na mpango unaoratibiwa na Marekani kuhusu Gaza nchini Israel, pamoja na maafisa wa ubalozi wa Uingereza walioko Ramallah, wanatakiwa kuondoka ndani ya siku saba, vyanzo hivyo viwili vilisema.
Waziri wa Mambo ya Nje Gideon Saar alisema Jumanne kuwa Uingereza lazima ifunge ubalozi wake mdogo Jerusalem Mashariki inayokaliwa, ambao una majukumu ya Mamlaka za Palestina, kulipiza vikwazo vya Uingereza kwa walowezi wa Kiisrael katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa Palestina.
Wengine waliochukua hatua kama hiyo ya Uingereza, ni Ufaransa na Canada ambao pia wamesema watapiga marufuku uagizaji wa bidhaa kutoka kwa eneo hilo la walowezi.
Serikali ya Israel, ambayo ilikuwa inatarajia vikwazo hivyo, itakutakana siku ya Jumatano kujadili hatua kwa nchi zilizotia saini hatua ya Uingereza, vyanzo hivyo vitatu vinavyofahamu suala hilo vilisema.
Vyanzo vyote vilizungumza kwa misingi ya kutotambuliwa.
Ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu haijatoa kauli yoyote kuhusu hilo.
Ufaransa na Sweden, ambao waliunga mkono hatua ya Uingereza, pia wana ubalozi mdogo Jerusalem Mashariki inayokaliwa kwa lengo la kuangazia Mamlaka ya Palestina.
Katika siku za nyuma Israel imelazimisha kufungwa kwa ofisi za ubalozi mjini Ramallah, katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa. Canada pia ina ofisi eneo hilo.




















