| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Algeria yaizuia UAE kutumia anga yake baada ya kusitisha uhusiano wa kidiplomasia
Wizara ya ulinzi ya Algeria inasema kuzuia matumizi ya anga kutaanza kutekelezwa Ijumaa, isipokuwa ndege za biashara kutoka uwanja wa ndege wa Algiers
Algeria yaizuia UAE kutumia anga yake baada ya kusitisha uhusiano wa kidiplomasia
Hatua hii ni kwa ndege zote za kiraia na kijeshi zilizosajiliwa UAE.

Algeria ilisema siku ya Alhamisi kuwa inazuia ndege zilizosajiliwa UAE kutumia anga yake baada ya kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na taifa hilo la Ghuba kufuatia mvutano wa muda mrefu.

Katika taarifa ya kutangaza kusitisha uhusiano wa kidiplomasia, Algeria imeishtumu nchi hiyo ya Ghuba "kwa vitendo vya kichokozi na uhasama", lakini haikusema wazi kuhusu kilichochochea.

Wizara ya ulinzi ya Algeria inasema marufuku ya kutumia anga itaanza kutekelezwa siku ya Ijumaa, isipokuwa kwa ndege za biashara kutoka uwanja wa ndege wa Algiers, ambazo zitaendelea na shughuli zake hadi mwisho wa 2026.

‘Juhudi zote za upatanishi zilokwama’

Nchi hiyo ya Afrika Kaskazini, ambayo kwa miezi kadhaa ilionesha ishara ya kusitisha uhusiano wa kidiplomasia, inasema uamuzi huo umejiri "baada ya njia zote za kuendeleza uhusiano wa mataifa hayo mawili kukwama" na UAE.

Wizara ya mambo ya nje ya UAE baadaye ilisema kuwa inatarajia kuwa uamuzi huo utakuwa wa muda tu ili kuendeleza "uhusiano wa karibu" na Algeria.

Wizara hiyo ya mambo ya nje ya Algeria inasema iliwaonya UAE lakini "wakaendelea na hali hiyo, hadi kufikia kiwango ambacho kisingeweza kukubalika au kuvumiliwa".

Siku ya Alhamisi, Algeria ilisema kuwa inampa balozi wa UAE saa 48 "kuheshimu uamuzi huo".

CHANZO:TRT Afrika Swahili