| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Wanafunzi 20 wafariki kufuatia moto ulioteketeza shule mashariki mwa DRC
Idadi ya waliokufa bado ni ya awali, hadi sasa chanzo cha moto huo hakijabainishwa.
Wanafunzi 20 wafariki kufuatia moto ulioteketeza shule mashariki mwa DRC
Inadaiwa kuwa moto huo ulianza katika jengo lililokuwa karibu na shule hizo kabla ya kuenea hadi kwenye shule. /

Wanafunzi wasiopungua 20 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya moto kuteketeza shule mbili mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku ya Alhamisi, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.

Tukio hilo limetokea katika shule za msingi za Ujamaa na Furaha, majira ya saa 8:00 asubuhi kwa saa za eneo, katika wilaya ya Chimpunda, Bukavu, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini, kwa mujibu wa UN Radio Okapi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, baadhi ya wanafunzi walifariki dunia katika msongamano uliotokea walipokuwa wakijaribu kujiokoa.

Watu wengine kadhaa waripotiwa kuwa katika hali mbaya wamelazwa katika vituo vya afya vilivyo karibu.

Inadaiwa kuwa moto huo ulianza katika jengo lililokuwa karibu na shule hizo kabla ya kuenea hadi kwenye shule.

Kwa sasa, Bukavu iko chini ya udhibiti wa kundi la waasi la AFC/M23.

Vyombo vya habari vya ndani pia viliripoti kuwa moto huo uliharibu takribani nyumba 500 pamoja na kliniki moja.

Hata hivyo, idadi ya waliokufa bado ni ya awali, na hadi sasa chanzo cha moto huo hakijabainishwa.

Tukio hilo limetokea siku chache baada ya watu 22 kuuawa na wengine kujeruhiwa baada ya moto kuzuka katika ukumbi wa harusi jijini Kinshasa, mji mkuu wa DR Congo.

CHANZO:AA