| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Ugonjwa wa Ebola wazidi kusambaa nchini DRC
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mlipuko huu unaenea kwa kasi zaidi kuliko milipuko yote ya Ebola iliyowahi kutokea, na tayari unachukuliwa kuwa mkubwa zaidi katika historia ya taifa hilo la Afrika ya Kati.
Ugonjwa wa Ebola wazidi kusambaa nchini DRC
Maambukizi ya Ebola huenea kupitia kugusa wanyama walio hai au waliokufa walioambukizwa au kwa kugusa ngozi au majimaji ya mwili wa mtu aliyeambukizwa

Ugonjwa wa Ebola unaendelea kusambaa ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC).

Kulingana na taasisi hiyo, ugonjwa wa Ebola ambao uliripotiwa kwa mara ya 17 nchini humo, Mei 15 mwaka huu, umeendelea kusambaa katika majimbo tofauti nchini humo.

Kufikia sasa, majimbo matani nchini humo yameendela kuripoti maambukizi ya ugonjwa wa Ebola.

Majimbo hayo ni pamoja na Ituri, Kivu Kaskazini, Kivu Kusini, Haut -Uele na Tshopo.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mlipuko huu unaenea kwa kasi zaidi kuliko milipuko yote ya Ebola iliyowahi kutokea, na tayari unachukuliwa kuwa mkubwa zaidi katika historia ya taifa hilo la Afrika ya Kati.

Hadi sasa, vifo zaidi ya 2,128 vimeripotiwa kati ya maambukizi 4,566 zilizothibitishwa, huku mikoa ya Ituri, Kivu Kaskazini, Kivu Kusini, HautUele na Tshopo ikiwa imeathirika kabla ya BasUele kuongezwa kwenye orodha.

Maambukizi ya Ebola huenea kupitia kugusa wanyama walio hai au waliokufa walioambukizwa au kwa kugusa ngozi au majimaji ya mwili wa mtu aliyeambukizwa ambaye ana dalili za ugonjwa huo.

Dalili zake ni pamoja na homa, maumivu ya misuli na mwili, maumivu ya kichwa, kikohozi, na koo linalouma, ikifuatiwa na kutapika na kuhara pamoja na kutokwa na damu mdomoni, puani, au viungo vya ndani.

CHANZO:AFP
Soma zaidi
Tanzania yaingia mkataba mpya wa kufadhili matibabu ya moyo kwa watoto zaidi ya 300
Seneta wa Kenya Boni Khalwale aomboleza kifo cha mkewe kutokana na mshtuko wa moyo
Morocco inaimarisha usalama huku kukiwa na wito wa watu wengi kuvuka mpaka kuingia Ceuta
Afrika Kusini 'imeaibishwa ' kutokana na mashambulizi dhidi ya wageni: Rais Ramaphosa
Zambia yasitisha zoezi la kuhesabu kura baada ya vurugu
Edwin Watenya Sifuna ni nani?
Zimbabwe yatangaza hali ya dharura kufuatia ajali ya kivuko huku idadi ya waliofariki ikifika 44
Jeshi la Sudan latibua mashambulizi ya ndege za RSF zilizolenga Khartoum na Mto Nile
Trump athibitisha kubadilisha ndege kufuatia vitisho vya Iran
Moto wazuka karibu na kiwanda cha kusafisha mafuta Libya baada ya mashambulizi
Ajali ya kivuko yaua 95 Zimbabwe
Kenya yapambana na wimbi la kauli za chuki, mwaka moja kuelekea Uchaguzi Mkuu
Tamasha la muziki la shule nchini Kenya lageuza mashindano kuwa sherehe za utamaduni
Wachimba migodi haramu wasiopungua 14 wafariki Afrika Kusini
Umoja wa Mataifa yaonya ukosefu wa usalama umewaondoa watu zaidi ya 5000 katika makazi yao Darfur
Watu 11 wauawa katika matukio tofauti ya ufyatuaji risasi Cape Town, Afrika Kusini
Siku ya Kimataifa ya Watu wa Asili: Ardhi, Utambulisho na mapambano ya kuhifadhi utamaduni
ISAYA YUNGE: Mjasiriamali wa Teknolojia kutoka Tanzania aliyemuoa binti yake Rais wa Kenya
Jimbo la Kano Nigeria laandaa harusi ya pamoja kwa wanandoa 1,500
Kizza Besigye: Kiongozi wa upinzani nchini Uganda 'anaumwa vibaya' arudishwa gerezani