| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Algeria yapitisha muswada wa adhabu ya kifo kwa wanaoanzisha moto wa nyika makusudi
Rais Tebboune alionya mwezi Agosti kuwa wale watakaohusika na kuanzisha moto wa nyika watakabaliwa na adhabu ya kifo.
Algeria yapitisha muswada wa adhabu ya kifo kwa wanaoanzisha moto wa nyika makusudi
Idadi rasmi ya waliofariki kutokana na moto wa nyika ni 12, lakini inaaminika huenda ikawa juu zaidi.

Wabunge nchini Algeria wamepitisha muswada wa kurejesha adhabu ya kifo kwa wale wanaoanzisha moto kwa makusudi kufuatia moto mkubwa wa nyika mwaka huu.

Muswada huo uliidhinishwa kwa kura 307-17 huku wabunge saba wakikosa kupiga kura siku ya Alhamisi. Algeria haijawahi kutekeleza huku ya kifo tangu 1993.

Rais Abdelmadjid Tebboune alionya mwezi Agosti kuwa wale watakaohusika na kuanzisha moto wa nyika watakabaliwa na adhabu ya kifo.

Zuio la hukumu ya kifo lilmekuwepo tangu 1993, mwaka ambao ilitekelezwa kwa mara ya mwisho kwa magaidi watatu waliopatikana na hatia ya mashambulizi ya kikatili katika Uwana wa Ndge wa Kimataifa wa Algiers.

Hukumu ya kifo

Muswada huo pia umeweka hukumu ya kifo kwa wanaoteka nyara watoto.

“Kuidhinishwa kwa muswada wa hukumu ya kifo kwa uhalifu huu ni hatua muhimu ya kisheria katika kuangamiza uhalifu huu,” Waziri wa Haki Lotfi Boudjemaa alisema.

Muswada huo uliungwa mkono na wahafidhina pia, ambao wana wabunge wengi bungeni. Hata hivyo, uamuzi huo, ulikashutumiwa na shirika la Amnesty International.

Idadi rasmi ya waliofariki kutokana na moto wa nyika ni 12, lakini inaaminika huenda ikawa juu zaidi, huku video kwenye mitandao ya kijamii zikionesha majeneza kadhaa yakiwa pembeni mwa makaburi ya halaiki mwezi uliopita.

Muswada huo utafanyiwa tathmini na Bunge la ngazi ya juu kabla kuidhinishwa rasmi.

CHANZO:TRT Afrika Swahili