| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Madaktari bingwa wa Tanzania waweka kambi ya matibabu Malawi
Lengo la kambi hiyo ni kutoa huduma za kibingwa katika upasuaji wa mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu, pamoja na matibabu ya magonjwa ya moyo na mfumo wa mkojo.
Madaktari bingwa wa Tanzania waweka kambi ya matibabu Malawi
Jopo hilo la madaktari wabobezi pia litasaidia katika kufanya tathmini kwa ajili ya upandikizaji wa figo. Picha/BMH

Madaktari bingwa kutoka nchini Tanzania, Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo jijini Dodoma, wameanza rasmi kambi ya matibabu nchini Malawi Septemba 28, itakayomalizika Oktoba 9, 2026.

Lengo la kambi hiyo ni kutoa huduma za kibingwa katika upasuaji wa mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu, pamoja na matibabu ya magonjwa ya moto na mfumo wa mkojo.

Jopo hilo la madaktari wabobezi pia litasaidia katika kufanya tathmini kwa ajili ya upandikizaji wa figo.

Kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Agnes Kayola, kambi hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi na Utalii wa Tiba yenye lengo la kuhakikisha upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa na wataalamu bingwa.

Wakati huo huo, kambi hiyo pia itatoa fursa ya kubadilishana uzoefu wa kimatibabu baina ya madaktari wa Tanzania na Malawi.

Kwa mujibu wa waandaaji, mwisho wa kambi hiyo kunatarajiwa kusainiwa Mkataba utakaowezesha wagonjwa wenye kuhitaji huduma zaidi kusafirishwa na kwenda Tanzania kupata huduma kulingana na mahitaji husika.

Soma zaidi