Uwanja wa ndege wa Istanbul umeweka rekodi mpya ya kupokea idadi kubwa ya ndege na abiria, kulingana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya Uchukuzi ya Uturuki.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara hiyo Agosti 16, uwanja huo, maarufu kama IGA Istanbul, umepokea abiria 290,287 na safari za ndege 1,739 hadi kufikia sasa.
Waziri wa uchukuzi wa nchi hiyo, Abdulkadir Uraloglu alisema uwanja wa ndege wa IGA Istanbul, unaendelea kuwa kitovu muhimu cha usafiri duniani.
ZILIZOPENDEKEZWA
“Uwanja huu unaendelea kuwa moja ya viwanja bora kabisa duniani, kwa huduma na hata miundombinu yake,” alisema Uraloglu.
CHANZO:Anadolu Agency





















