| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Tanzania: Gharama za petroli zazidi kupungua
Kulingana na EWURA, kwa sasa petroli itauzwa kwa Dola 1.46 (Shilingi 3,898) dizeli Dola 1.50 (Shilingi 3,978) kwa lita, kufuatia marekebisho hayo ya be.
Tanzania: Gharama za petroli zazidi kupungua
Mabadiliko ya gharama hizo, pia zitashuhudiwa katika mikoa ya Arusha, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Tanga na Kigoma.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Tanzania(EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta ya petroli, dizeli na taa, ambapo zote zimeshuka kuanzia kipindi kipya cha bei.

Kwa mujibu wa taarifa ya EWURA, bei mpya zilizoanza kutumika Agosti 5, 2026, zimepungua kwa Dola 0.035 (Shilingi 92) kwa lita moja ya petroli, Dola 0.077 (Shilingi 204) kwa lita moja na Dola 0.17 (Shilingi 440) kwa lita ya mafuta ya taa ikilinganishwa na mwezi Julai, kufuatia kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia.

Kulingana na EWURA, kwa sasa petroli itauzwa kwa Dola 1.46 (Shilingi 3,898) dizeli Dola 1.50 (Shilingi 3,978) kwa lita, kufuatia marekebisho hayo ya bei yaliyotangazwa na mamlaka hiyo.

Mabadiliko ya gharama hizo, pia yatashuhudiwa katika mikoa ya Arusha, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Tanga na Kigoma.

EWURA imesema mabadiliko hayo yametokana na mwenendo wa soko la kimataifa, huku ikiwataka wafanyabiashara kuuza mafuta kwa bei zisizozidi kiwango kilichotangazwa na kuweka mabango ya bei sehemu zinazoonekana na wateja.

"Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yeyote atakayekiuka agizo hili," ilisema EWURA katika taarifa yake.

Mamlaka hiyo imewahimiza wananchi kuhakiki bei za mafuta katika maeneo yao kwa kutumia huduma ya simu ya mkononi na kudai stakabadhi za mauzo ili kurahisisha ufuatiliaji wa malalamiko endapo mafuta yatauzwa zaidi ya bei kikomo iliyotangazwa.

CHANZO:TRT Afrika Swahili