Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa richa 5.0 lilipiga mkoa wa Malatya, uliopo upande wa mashariki wa Uturuki, mapema Jumamosi, kulingana na Mamlaka ya Usimamizi wa Maafa na Dharura (AFAD).
Tetemeko hilo lilitokea saa kumi na mbili na dakika ishini alfajiri kwa saa za eneo hilo (0320 GMT), katika wilaya ya Battalgazi kwa kina cha kilomita 15.59 (maili 9.69), AFAD ilisema.
Tetemeko lilisikika pia katika mikoa jirani ya Elazig, Adiyaman, Tunceli na Sanliurfa.
AFAD ilisema hakukuwa na ripoti za papo hapo za uharibifu au vifo kufuatia tetemeko hilo.
Murat Kurum, Waziri wa Mazingira, miji na mabadiliko ya tabianchi, pia alisema kupitia mtandao wa kijamii wa Uturuki, NSosyal: "Baada ya tetemeko la Battalgazi, hadi sasa hatujapata dalili za madhara, lakini tunapitia ripoti zote."


















