| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Rais wa Misri kufanya ziara ya siku mbili Tanzania
Rais El-Sisi na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan wanatarajiwa kujikita zaidi katika kuimarisha biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili, pamoja na kujadili masuala ya ulinzi wa kikanda.
Rais wa Misri kufanya ziara ya siku mbili Tanzania
Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada pana za kudumisha ushirikiano kati ya Misri na Tanzania.

Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi anatarajiwa kufanya ziara rasmi ya siku mbili nchini Tanzania itakayoanza Julai 20, 2026.

Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada pana za kudumisha ushirikiano kati ya Misri na Tanzania.

Rais El-Sisi na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan wanatarajiwa kujikita zaidi katika kuimarisha biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili, pamoja na kujadili masuala ya ulinzi wa kikanda.

Ziara hiyo inaelezwa na wachambuzi wa masuala ya diplomasia kuwa ni muhimu katika kudumisha ushirikiano wa kidiplomasia na kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya Tanzania na Misri.

Mara ya mwisho kwa Rais El-Sisi kuitembelea Tanzania ilikuwa ni Agosti 17, 2017, ambapo alikutana na mwenyeji wake aliyekuwa Rais wa nchi hiyo wakati huo Hayati John Pombe Magufuli.

Mazungumzo yao yalijikita zaidi katika kuongeza ushirikiano wa kibiashara, na kukamilisha utiaji saini wa mikataba mikubwa ya miundombinu.

Itakumbukwa kuwa, baadhi ya makampuni ya Misri yanahusika katika ujenzi wa miundombinu mikubwa nchini Tanzania ikiwemo mradi wa uzalishaji umeme kutoka Bwawa la Mwalimu Nyerere wenye thamani ya Dola bilioni 2.9.