Waziri wa Uturuki wa Mambo ya Nje Hakan Fidan amesema jaribio la mapinduzi lililofeli Julai 15, 2016 limeonesha kwamba Uturuki haiwezi kusalimu amri kwa mashirika ya kigaidi.
Katika ujumbe wa maadhimisho ya Siku ya Demokrasia na Umoja wa Kitaifa, Fidan amesema Julai 15 ilikuwa ni siku ambayo Uturuki ilitangaza kwa dunia kwamba nia yake ya utaifa haingetii "nguvu yoyote ya usimamizi wa kulazimisha, mtandao wowote wa uhaini, au njama yoyote potofu."
Amesema jaribio la mapinduzi la Shirika la Kigaidi la Fetullah (FETO) lilitibuliwa kupitia "uongozi wenye ari wa Rais Recep Tayyip Erdogan, ari isiyotetereka ya taifa letu, na utashi usioyumbishwa wa taifa."
Vifaru na silaha haziweshi kunyamazisha watu wa Uturuki
Fidan amesema walioamini vifaru, silaha na vitisho kwamba vinaweza kunyamazisha watu wa Uturuki walishindwa na mamilioni ya watu waliojitokeza barabarani kulinda nchi yao.
"Ari ya kuungana na umoja uliyooneshwa usiku ule ulitibua njama zote dhidi ya Uturuki," amesema.
Ameongeza kwamba mapambano ya Uturuki dhidi ya tishio la usalama wake, uhuru na amani ya umma yanaendelea nyumbani na nje ya nchi kwa ari ile ile.
"Katu hatutaruhusu mashirika ya kigaidi kukaa katika nchi yoyote, taasisi au mfumo," amesema Fidan.
Waziri wa Mambo ya Nje pia amewaenzi wale waliouawa katika jaribio la mapinduzi na kuwashukuru maveterani, na kulitakia taifa maadhimisho mema katika Siku ya Demokrasia na Umoja wa Kitaifa.



















