| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
ECOWAS yaunga mkono mradi wa bomba la gesi kati ya Nigeria na Morocco
Mradi huo wa bomba, ulitiwa saini muongo mmoja uliopita kati ya Mfalme wa Morocco na rais wa Nigeria.
ECOWAS yaunga mkono mradi wa bomba la gesi kati ya Nigeria na Morocco
Mradi wa bomba la gesi utasafirisha gesi asilia kutoka Nigeria kupitia nchi 13 za Afrika Magharibi hadi Morocco.

Wanachama wa Jumuia ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) imesaini makubaliano ya kiserikali Jumapili katika mji wa Freetown yanayounga mkono mradi wa gesi wa Atlantiki kati ya Nigeria na Morocco. Hayo ni mwa mujibu wa taarifa ya pamoja ya Morocco na Nigeria.

Mradi huo wa bomba la gesi umesanifiwa kusafirisha mita za mraba za gesi asilia bilioni 30 kwa mwaka kutoka Nigeria na Afrika Magharibi kupitia nchi 13 kwenda Morocco, hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya pamoja ya Shirika la Madini la Morocco (ONHYM) na Shirika la Mafuta la Serikali la Nigeria (NNPC).

Kwa kiwango hicho, mita za mraba bilioni 15 zitakuwa ni kwa ajili ya Morocco na masoko ya Ulaya kupitia bomba ambalo tayari linaunganisha Morocco na Hispania, imesema taarifa.

Mradi huo wa bomba, ulitiwa saini muongo mmoja uliopita kati ya Mfalme wa Morocco na rais wa Nigeria, utakuwa na urefu wa kilomita 6'900 kupitia baharini na nchi kazi na unakisiwa kugharimu kiasi cha Dola bilioni 25.

Mradi huo ulikamilisha hatua zake wa utafiti na uwezekano wa usanifu wa awali wa kiuhandisi (FEED).

Mwezi Aprili, ONHYM iliiambia Reuters kwamba mradi huo una lengo la kujumuisha ushirikiano kati ya nchi za Afrika Magharibi kwa kuongeza uzalishaji wa nishati ya umeme na kuwezesha ukuaji wa viwanda na sekta ya madini, huku ikiisaidia Morocco kuwa daraja la nishati kati ya Afrika na Ulaya.

Hatua inayofuata itakuwa ni kutia saini makubaliano kati ya Morocco na Mauritania yatakayohudhuriwa na rais wa Nigeria, imeongeza kusema taarifa hiyo.