Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa amesitisha shambulio lililopangwa dhidi ya Iran baada ya kusema kuwa muundo wa makubaliano ulikuwa umeafikiwa, huku akiweka sharti kwamba makubaliano ya haraka yafikiwe.
Katika taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa Truth Social, Trump alisema Marekani ilikuwa tayari kuanzisha shambulio dhidi ya Iran lakini iliombwa na Iran pamoja na nchi nyingine za Mashariki ya Kati kusitisha hatua hiyo.
Alisema kuwa muundo wa makubaliano utajumuisha kufunguliwa upya kwa Mlango Bahari wa Hormuz "mara moja na kwa ukamilifu" pamoja na "kukomesha tishio la nyuklia la Iran."
"Kufuatia ombi hili, nimekubali — kwa ajili ya manufaa ya baadaye ya DUNIA na pia kwa ajili ya ustawi na mafanikio ya Iran — kusitisha shambulio hilo, iwapo itawezekana kufikia MAKUBALIANO ya haraka," alisema Trump.
Pia alisema kuwa Israel "inaungana nami katika ahadi hii."
Trump aliongeza kuwa Marekani ilikuwa "imejiandaa kikamilifu na kuwa tayari kuchukua hatua" dhidi ya Iran kabla ya kuamua kusitisha shambulio lililopangwa.





















