| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Jamhuri ya Afrika ya Kati yafunga mgodi wa dhahabu baada ya watu kufariki
Juhudi za uokoaji zilisitishwa kutokana na mgodi kutitia na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.
Jamhuri ya Afrika ya Kati yafunga mgodi wa dhahabu baada ya watu kufariki
Mgodi kama huo wa dhahabu wa Be-Mbari, pia karibu na mpaka wa Cameroon, ulisababisha vifo vya watu kadhaa mwezi Juni.

Jamhuri ya Afrika ya Kati imefunga kwa muda mgodi wa dhahabu karibu na mpaka wa Cameroon baada ya maporomoko ya ardhi kusababisha vifo vya watu kadhaa mapema wiki hii, waziri wa madini wa nchi hiyo alisema siku ya Alhamisi.

Rufin Benam-Beltoungou alitembelea mgodi wa Zamboye siku ya Jumatano na kueleza kuwa idadi rasmi ya waliofariki ni 49, wizara iliiambia AFP.

Waziri huyo alithibitisha kuwa watu hao ni pamoja na raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati 34, 13 kutoka Cameroon na raia wawili wa Chad.

Vyanzo kadhaa vya eneo hilo viliiambia AFP kuwa watu karibu walifariki, huku wakiwa hawajulikani waliko na pengine wamefukiwa na kifusi.

Watu saba waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali ya karibu ya mji wa Baboua, karibu umbali wa kilomita 50.

Maafisa wa usalama wanalinda migodi

Mgodi huo ulikuwa umefungwa na watu walizuiwa kufika huko siku ya Alhamisi, mwandishi wa AFP aliripoti.

Maafisa zaidi wa usalama walipelekwa, ikiwemo wale kutoka kundi la wapiganaji la Urusi la Wagner.

Juhudi za uokoaji zilisitishwa kutokana na kuendelea kutitia kwa mgodi na mvua kubwa kuendelea kunyesha.

Waziri wa madini anasema mkasa huo unadhihirisha hatari za uchimbaji haramu wa madini, "hasa katika maeneo ambayo yana viwango vidogo vya usalama".

Kuporomoka kwa migodi katika taifa la Jamhuri ya Afrika ya Kati hutokea mara kwa mara, ambapo kuna dhahabu na madini mengine yanayochimbwa kwa njia haramu na serikali haina utaratibu wa kuratibu.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Soma zaidi
Mkuu wa Umoja wa Mataifa asikitishwa kwa kunyimwa viza  kiongozi wa Sudan, Burhan kuhudhuria UNGA
Jenerali wa DR Congo miongoni mwa watu 13 waliofariki katika ajali ya ndege
Afrika itapata hadhi ya uwanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa?
Sudan yashtumu taarifa za Marekani zinazohoji uhalali wa serikali huku viza ya Burhan ikizua utata
Mke wa Besigye awataka viongozi wa Afrika wazungumzie masuala ya haki za binadamu
Waasi wa Tigray 'wadhibiti' uwanja wa ndege wa kanda ya Ethiopia
Tanzania yatoa wito wa amani Gaza
Sudan yaahidi kukabiliana na mfumuko wa bei huku vita vikiathiri uchumi
Makundi saba yenye silaha yaunda muungano nchini Ethiopia
Afrika Kusini yawakamata washukiwa watatu baada ya miili tisa wanawake kupatikana
9 wauawa kwa kupigwa risasi katika Jimbo la Plateau nchini Nigeria
Jeshi la Namibia lakumbwa na shambulio la mtandaoni
Simba kumi wakutwa wamekufa katika hifadhi ya Ngorongoro nchini Tanzania
Kuanzia watoto watano hadi mapambano ya kuishi: Changamoto ya uzazi wa watoto wengi barani Afrika
Jeshi la Sudan lawaua wapiganaji wa RSF na kuharibu magari tisa katika eneo la Blue Nile
Mswada mpya Sudan Kusini kumpa Salva Kiir mamlaka yote ya kuwafuta kazi Makamu wake kabla uchaguzi
Sudan Kusini inasonga mbele na mipango ya mradi wa Bwawa la Grand Fula kwenye mto White Nile
Marekani inatuma dola milioni 2.5 nchini Gambia kutokana na mauzo ya kasri la rais wa zamani
Afrika Kusini yatoa zawadi ya $24,600 kwa taarifa kuhusu muuaji wa wanawake
TikTok kukata kodi kwenye mapato ya waandaaji maudhui Kenya