Sudan imeshtumu taarifa za Marekani zinazohoji uhalali wa serikali yake, ikitoa wito kwa Marekani kutoa ushirikiano mzuri kwa Sudan, huku kukiwa na utata kuhusu viza ya Umoja wa Mataifa ya Mwenyekiti wa Baraza la Sudan Abdel Fattah al Burhan ikiongeza uhasama kati ya mataifa hayo mawili.
Wizara ya mambo ya nje ya Sudan ilisema siku ya Jumatano kuwa Sudan “inaheshimu uhuru wa taifa lake” na inashtumu vikali taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ambayo imekataa kutambua uhalali wa Jeshi la Sudan kuhusu utawala wa kikatiba.
Wizara inasema kuwa mpango wa amani lazima uheshimu uhuru wa Sudan, umoja, na taasisi za kitaifa, wakati ikigusia kile walichokitaja kuwa uingiliaji wa mataifa ya nje katika mgogoro huo.
Taarifa hiyo imekuja baada ya ripoti kuibuka kuwa Marekani ilikuwa inazuia viza ya Burhan wakati akijiandaa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa na amewekewa masharti ya kukubali kusitisha mapigano kwa siku 90 ili aweze kupewa viza hiyo.
Sekretariati ya Umoja wa Mataifa imetaka kupewa maelezo na Marekani kuhusu suala hilo.



















