| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Watu wasiopungua 40 wafariki katika ajali ya boti jimbo la Sokoto nchini Nigeria
Boti lilizama katika jimbo la kaskazini magharibi la Sokoto nchini Nigeria, miili 40 ya watoto imepatikana kufikia sasa, afisa mmoja wa eneo hilo alisema siku ya Alhamisi.
Watu wasiopungua 40 wafariki katika ajali ya boti jimbo la Sokoto nchini Nigeria
Watu wasiopungua 40 wamefariki baada ya boti lao kuzama katika jimbo la Sokoto kaskazini magharibi mwa Nigeria Agosti 20, 2026.

Boti limezama katika jimbo la kaskazini magharibi mwa Nigeria la Sokoto, huku miili karibu 40 ya watoto ikipatikana kufikia sasa, afisa mmoja wa mamlaka ya bandari alisema siku ya Alhamisi.

"Naweza kuthibitisha kuwa kufikia sasa miili karibu 40 ya watoto imepatikana," Abdulkadir Yusuf, meneja wa Mamlaka hiyo alisema katika taarifa kwa Reuters.

Ajali hiyo ilitokea Alhamisi asubuhi wakati abiria, waliokuwa kwenye boti hiyo inayosemekana ilikuwa na abiria zaidi ya kiwango chake, walikuwa wanavuka kwa ajili ya shughuli za kilimo au kuvuna mpunga,alisema Sarkin Daji, kiongozi wa eneo hilo.

"Wapiga mbizi wetu wamepata miili na bado shughuli za kutafuta zinaendelea," mkazi wa eneo hilo Nasiru Gorau alisema.

Mwezi Januari, watu wasiopungua 25 walifariki wakati boti lililokuwa likivuja lilipozama katika jimbo la Yobe, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

CHANZO:TRT Afrika Swahili