| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Mkuu wa Ujasusi wa Ecuador, mkewe miongoni mwa watu saba waliofariki katika ajali ya helikopta Kenya
Mkuu wa ujasusi wa Ecuador Michele Sensi-Contugi na mkewe, Stephany Hollihan Vasconez, ni miongoni mwa watu saba waliofariki katika ajali ya helikopta nchini Kenya siku ya Jumatano, serikali ya Ecuador ilitangaza.
Mkuu wa Ujasusi wa Ecuador, mkewe miongoni mwa watu saba waliofariki katika ajali ya helikopta Kenya
Mkuu wa Ujasusi wa Ecuador Michele Sensi-Contugi na mkewe wamefariki katika ajali ya helikopta nchini Kenya Agosti 19, 2026.

Mkuu wa ujasusi wa Ecuador Michele Sensi-Contugi na mkewe, Stephany Hollihan Vasconez, ni miongoni mwa watu saba waliofariki katika ajali ya helikopta nchini Kenya siku ya Jumatano, serikali ya Ecuador ilitangaza. "Leo Michele na Stephany wameaga dunia. Tunawafariji familia yao, hasa watoto na wazazi wao," Waziri wa Uchukuzi wa Ecuador Roberto Luque aliandika kwenye mtandao wa X.

Ajali hiyo ilitokea Mlima wa Ololokwe Kaunti ya Samburu, karibu kilomita 270 kaskazini mwa mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Raia mwingine wa Italia na Ecuador pia alikuwa miongoni mwa waliofariki katika ajali hiyo ya Jumatano, vyombo vya habari vya Italia vilisema.

Walikuwa wanatalii nchini humo wakati helikopta yao ilipopata ajali, huku chanzo cha ajali hiyo kikiwa bado hakijabainika.

Mfanyabiashara maarufu

Michele Sensi-Contugi, 44, alikuwa mfanyabiashara maarufu wa Ecuador na mkuu wa shirika la ujasusi. Miongoni mwa biashara zake ilikuwa ni pamoja na ndege za kitalii, pamoja na kutengeneza bidhaa za plastiki.

Sensi-Contugi alizaliwa eneo la Desio, katika mkoa wa Monza-Brianza huko Italia, Agosti 12, 1982. Baba yake ni raia wa Italia na mama yake ni kutoka Ecuador.

Sensi-Contugi aliimarisha biashara yake katika sekta ya viwanda kabla ya kuwa afisa mwandamizi serikalini.

Alikuwa maarufu zaidi katika siasa 2024 kipindi cha Rais Daniel Noboa, alipokuwa kaimu waziri kati ya mwezi Aprili na Agosti 2024 kabla ya kuteuliwa mkurugenzi mkuu wa shirika la ujasusi la Ecuador.

Mke wake, Stephany Hollihan Vasconez, ambaye pia alifariki katika ajali hiyo ya helikopta, alikuwa mwanamitindo maarufu nchini Ecuador, na alikuwa anafahamika katika sekta ya mitindo ya nchini humo.

Awamu ya Sensi-Contugi kuwa mkuu wa shirika la ujasusi Ecuador imekuja wakati ambao serikali ya Noboa imelipa kipaumbele suala la usalama na ukusanyaji wa taarifa za kijasusi katika juhudi za kukabiliana na tatizo la usalama usalama nchini humo.

CHANZO:TRT Afrika