| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Australia yathibitisha vifo vya ndege vinavyotokana na mafua H5
Mamia ya ndege mwitu wamepatikana wamekufa katika pwani ya Kusini mwa Australia huku seerikali ikitahadharisha uwezekano wa vifo zaidi. Hakuna maambikizi kwa kuku.
Australia yathibitisha vifo vya ndege vinavyotokana na mafua H5
Serikali nchini humo imesema kunaweza kuwa na ongezeko la vifo vya ndege kutokana na mafua H5.

Australia imethibitisha vifo vya ndege mwitu waliofariki kutokana na ugonjwa wa mafua wa H5, baada ya idadi kubwa ya korongo kuonekana wamekufa na wengine wanaumwa katika kisiwa Kusini mwa Australia, vyombo vya habari vya nchi hiyo vimeripoti Jumatatu.

Ndege hao wameonekana kutoka angani katika eneo la majabali la Baudin, takriban kilomita 5 kusini mwa Cape Jaffa, Ijumaa.

Vipimo vya sampuli baadae vilionesha maambulizi ya avian H5, kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji wa Australia (ABC).

Australia, ni bara la mwisho kutokuwa na maambukizi ya virusi mpaka kufikia Julai 14, mara ya mwisho limerekodi maambukizi ya mafua ya H5 kutoka kwa ndege wa baharini wanaosafiri hasa aina ya petrel, katika fukwe ya Kusini mwa Australia, Magharibi mwa Australia na New South Wales.

Nchi hiyo hivi sasa imerekodi maambukizi 74 yaliyothibitishwa, ikiwemo 54 Kusini mwa Australia, 10 Magharibi mwa Australia, saba eneo la Victoria, mawili New South Wales na moja Queensland.

Maafa yanatarajiwa kwa wanyamapori

Waziri wa Kilimo Julie Collins amesema idadi kubwa ya vifo ilitarajiwa.

"Kwa masikitiko, tunajua kwamba mafua ya H5 yanaenea kupitia moto wa porini na mazingira asilia, haiwezekani kuzuia vifo," amesema.

Collins amesisitiza kuwa hakuna uthibitisho kwamba virusi vimeenea kwa kuku au katika mashamba ya biashara na kusema kuwa hatari kwa binadamu bado ni ndogo.

Waziri wa Mazingira Murray Watt amewatahadharisha raia wa nchi hiyo kwamba watarajie mlipuko zaidi utakaoathiri wanyamapori.

"Huwezi kuzuia ndege kuruka, na huwezi kuzuia wanyamapori kuzunguka, na hiyo ina maana hasara zaidi kama tunayoshuhudia sasa," amesema.

Mamlaka nchini humo imeanzisha mpango wa taifa wa dharura wa kukabiliana na H5, ikichangiwa na ongezeko la fedha kiasi cha Dola milioni 15.5 kutoka serikali kuu na majimbo.