Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amefanya mazungumzo ya simu na Rais Edgars Rinkevics wa Latvia, na kujadiliana masuala mbalimbali, yakiwemo uhusiano ndani ya NATO, masuala ya kikanda na kiulimwengu.
Katika mazungumzo hayo ya siku ya Jumanne, Erdogan alisema Uturuki inatambua umuhimu mkubwa wa ulinzi wa eneo la Baltiki, kulingana na taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano yay a Uturuki, kuwekwa kwenye mtandao wa kijamii wa NSosyal.
Erdogan alionesha kufurahishwa kuwa mwenyeji wa Rinkevics nchini Uturuki hasa wakati wa mkutano wa NATO, akionesha matumaini kuhusiana na maamuzi yaliyofikiwa wakati wa mkutano huo mkubwa wa kihistoria.
Kiongozi huyo, pia alionesha hamu yake kukuza ushirikiano kati ya Uturuki na Latvia, katika nyanja mbalimbali zikiwemo ulinzi.



















