| Swahili
Maoni
AFRIKA
3 dk kusoma
Vijana wa Afrika wanataka kutambuliwa. Wakati ni sasa
Vijana wa Afrika siyo tu wanasubiri sera zipitishwe; wanatoa muelekeo katika bara kupitia uanaharakati, ujasiriamali, na umoja. Swali si kuwa kama vijana wako tayari. Ni kama viongozi barani Afrika wako tayari.
Vijana wa Afrika wanataka kutambuliwa. Wakati ni sasa
Maandamano yaliyoongozwa na vijana nchini Kenya dhidi ya muswada tata wa fedha ulisababisha vifo vya watu kadhaa. / AFP

Na Cindy Kasanga

Vijana barani Afrika wameitwa kuwa raslimali kubwa lakini kauli hiyo imepoteza maana. Rasilimali zinatakiwa kuhusishwa katika uwekezaji — lakini nani anafaidi wakati hilo linakuwa halifanyiki?

Idadi ya vijana barani Afrika inatazamiwa kuongezeka kwa milioni 132 muongo huu. Idadi kubwa ya vijana siyo sehemu ya mkakati.

Sababu ni ya kisiasa. Uchumi wa mataifa ya Afrika, kama ilivyo kwa mifumo ya sasa hivi, hayatoi fursa kwa vijana wake kuchangia katika kazi zenye tija. Wengi wanatengwa katika maeneo ya kutoa maamuzi.

Maandamano ya hivi majuzi ya vijana yalidhihirisha tatizo hili. Nchini Kenya,maandamano dhidi ya Muswada wa Fedha ambao uliongeza kodi kwa bidhaa za misingi yalionesha ghadhabu kwa serikali ambayo iliahidi ahuweni lakini ikaishia kuwapa watu dhiki.

Nchini Madagascar, kukatika kwa umeme na kukithiri kwa umaskini kulifanya vijana waingie barabarani kutaka mabadiliko. Huko Morocco, hasira za vijana ni kuhusu fedha kidogo kwa ajili ya shule na hospitali huku serikali ikianikwa kwa kulipa kipaumbele suala la viwanja kuliko huduma za kijamii. Kote barani, upinzani wa vijana unaonesha jambo moja: kutengwa kwao kisiasa.

Vijana hawana nafasi

Kwa kuwa tabaka za wazee ndilo limejikita zaidi kwenye siasa, ikiwa ni muenendo uliokuwepo tangu kuondoka kwa wakoloni. Pamoja na serikali nyingi kuahidi kujumuisha vijana, lakini hali ni tofauti.

Wakati huo huo, ufisadi unaendelea kumaliza rasilimali ambazo zingesaidia kubadilisha maisha ya vijana. Afrika inapoteza Dola bilioni $9 kila mwaka kwa tatizo la usimamizi mbaya wa fedha — pesa ambazo zingetumika kufadhili shule, ajira, na miundombinu ambayo vijana wengi wanataka. Ufisadi unasababisha hali ya kutojali, kudhoodisha taasisi, na kuondoa uaminifu kati ya serikali na raia.

Kiuchumi, hali ni mbaya. Sekta isio rasmi inasaidia karibu asilimia 70% ya familia barani Afrika na kutoa ajira kwa vijana. Mara nyingi kazi hizi zinakuwa si za kudumu, na mshahara wake ni mdogo. Asilimia tisini ya vijana wanafanya kazi katika sekta isiyo rasmi, na thuluthi moja wanaishi katika hali ya umaskini licha ya kuajiriwa. Kwa kifupi, kuwa kazi siyo hakikisho la kuondokana na umaskini.

Wakati wa kujumuishwa sasa

Maandamano yaliyokuwepo kote barani siyo tu ni jambo la kupita lakini ni mitazamo kwa serikali ambazo zinazungumzia kuhusu uwezo wa vijana bila ya kutekeleza. Baadhi ya vijana wameuawa wakitetea haki hii — jambo lisilokubalika katika jamii inayodai kuhesimu mustakabali wao.

Vijana wa Afrika siyo tu wanasubiri sera zipitishwe; wanatoa muelekeo katika bara kupitia uanaharakati, ujasiriamali, na umoja. Swali si kuwa kama vijana wako tayari. Ni kama viongozi barani Afrika wako tayari.

kinachotakiwa kufanywa: marekebisho katika uchumi ambao unawaweka vijana katika hatari, na kukasimu mamlaka ili wasiwe kimtya. Vipaumbele viwili hivi haviwezi kutenganishwa. 

Kwa muda mrefu vijana wameahidiwa fursa. Ni wakati wa utekelezaji sasa.

Mwandishi, Cindy Kasanga, ni mtafiti anayesoma Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha British Columbia. Amezaliwa na kulelewa nchini Kenya na Ethiopia, utafiti wake unaangazia suala la usawa, madaraka, na mfumo wa taasisi katika uhusiano wa kimataifa, akiangazia barani Afrika.

CHANZO:TRT Afrika
Soma zaidi
Waburundi waomba nyaraka za kusafiria kufuatia operesheni dhidi ya wafanyabiashara wa kigeni Kenya
Watu wawili wafariki, wengine 25 wajeruhiwa baada ya basi la mahujaji wa Misri kupata ajali Makkah
Mume wa Rais Samia wa Tanzania afariki dunia
Cabo Verde yatangaza maombolezo ya kitaifa baada ya vifo vya watoto katika ajali ya basi
Mlipuko wa kipindupindu, Kordofan Magharibi umesababisha vifo vya watu 23
Romanda Hombir wa Afrika Kusini ashinda taji la Miss World Africa 2026
DRC inachunguza ajali mbaya ya moto katika sherehe ya harusi ulioua wageni 22
Unyanyasaji kwa wazee janga linaloenea kimya kimya
Marekani kuondoa ufadhili wa Dola milioni 45 za VVU kwa Namibia
Niger yaishutumu Ufaransa kwa jaribio lililofeli la uasi wa kijeshi
Huduma ya Kitaifa ya Polisi ya Kenya (NPS) inatoa onyo kwa wanasiasa kabla ya uchaguzi mkuu
Marekani yaongeza muda wa AGOA hadi mwisho wa 2028
Marekani inashinikiza kusitishwa kwa mapigano kwa sababu za kibinadamu bila vikwazo nchini Sudan
UN yapiga kura kuidhinisha ramani ya dunia inayoonyesha ukubwa halisi wa Afrika
Mfalme Oyo Nyimba: Mwili wa mfalme mdogo zaidi warudishwa Uganda kwa mazishi
Raia wa Marekani waokolewa baada ya mashambulizi katika kambi ya mbuga ya wanyamapori Msumbiji
Air Tanzania kuanza tena safari za Moscow Septemba 7 baada ya kusitisha kwa muda
Air Tanzania yasitisha safari za Moscow kwa sababu za kiusalama
Ripoti ya UN yalaumu mitandao ya kigeni kwa kuchochea vita vya Sudan
Mashambulizi ya RSF kwa UN Kordofan Kusini Sudan yasababisha kifo cha mtu mmoja, wawili wajeruhiwa