| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Taifa la Nauru labadilisha jina, sasa kuitwa Naoero
Uamuzi wa kubadili jina la taifa hilo, ulifikiwa mwezi Januari, kupitia muswada maalumu wa mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo.
Taifa la Nauru labadilisha jina, sasa kuitwa Naoero
Uamuzi wa kubadili jina la taifa hilo, ulifikiwa mwezi Januari, kupitia muswada maalumu wa mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo.

Nauru imebadili rasmi jina lake na kwa sasa, taifa hilo litafahamika kama Jamhuri ya Naoero.

Kulingana na serikali ya taifa hilo dogo linalopatikana katika kisiwa cha Pasifiki, kifupi cha utambulisho mpya wa taifa hilo, sasa utakuwa NRO.

Uamuzi wa kubadili jina la taifa hilo, ulifikiwa mwezi Januari, kupitia muswada maalumu wa mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo.

Hata hivyo, ilibidi kusubiri kwa siku 90 ili uamuzi huo uidhinishwe na bunge la nchi hiyo, ambapo, spika wa nchi hiyo Marcus Stephen aliyaidhinisha Mei 13.

Kulingana na Rais David Adeang, mabadiliko hayo hayakufikiwa kisiasa, bali kwa kutambua uruthi na utamaduni wa taifa hilo.

“Naoero ni mwanzo wa ukurasa mpya, fahari yetu mpya na maendeleo endelevu,” alisema kiongozi huyo.

CHANZO:Anadolu Agency