| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Wapalestina kufanya uchaguzi wa rais na wabunge
Abbas na Mamlaka ya Palestina, wapo katika shinikizo kubwa kutoka kwa Marekani, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Nchi za Kiarabu, ya kuleta mageuzi na kuendesha uchaguzi, huku taifa hilo likikabiliwa na kudumaa kwa siasa na uwepo wa tuhuma za ufisadi.
Wapalestina kufanya uchaguzi wa rais na wabunge
Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ameahidi kufanya mageuzi ndani ya mamlaka ya Palestina./Picha:Reuters / Reuters

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ameahidi kufanya mageuzi ndani ya mamlaka ya Palestina, wakati taifa hilo likijiandaa na uchaguzi wa rais na wabunge.

Haya yanajiri wakati chama cha Fatah kimefanya mkutano wa siku tatu kuchagua kamati kuu kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 10.

"Tunaahidi kutekeleza ahadi za mageuzi na tupo tayari kufanya uchaguzi wa rais na wabunge," alisema Abbas.

Abbas na Mamlaka ya Palestina, wapo katika shinikizo kubwa kutoka kwa Marekani, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Nchi za Kiarabu, ya kuleta mageuzi na kuendesha uchaguzi, huku taifa hilo likikabiliwa na kudumaa kwa siasa na uwepo wa tuhuma za ufisadi.

Kamati Kuu ya chama cha Fatah inatarajiwa kuwa kiungo muhimu mara baada ya utawala wa Abbas kufikia kikomo, huku wachunguzi wa mambo wakijiuliza kama ataachia ngazi baada ya kuwepo madarakani kwa zaidi ya miongo miwili bila uwepo wa mrithi wake.

CHANZO:AFP