| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Wanajeshi wa Nigeria wawaokoa waliotekwa na magaidi wa Boko Haram
Waliookolewa ni pamoja na wanaume 52, wanawake 33 na watoto 7, jeshi limesema.
Wanajeshi wa Nigeria wawaokoa waliotekwa na magaidi wa Boko Haram
Ugaidi wa Boko Haram ulianza 2009 kaskazini mashariki mwa Nigeria. / Reuters

Mamlaka za Nigeria zimewaokoa raia 92 ambao walikuwa wametekwa na makundi ya kigaidi ya Boko Haram na Daesh.

Luteni Kanali Sani Uba, afisa habari wa operesheni Hadin Kai, kikosi cha jeshi cha kukabiliana na ugaidi, amesema katika taarifa siku ya Jumapili kuwa jeshi lilifanya operesheni dhidi ya Boko Haram na Daesh jimbo la kaskazini mashariki la Borno.

Uba anasema watu 92 waliokuwa wametekwa na magaidi wameokolewa wakati wa operesheni hiyo.

Aliongeza kuwa mifumo ya uchunguzi ilisaidia kufanikisha uokoaji huo.

“Waliookolewa ni pamoja na wanaume 52, wanawake 33 na watoto saba," alisema.

Kwa muda mrefu Nigeria imekabiliwa na mashambulizi ya magenge yenye silaha pamoja na makundi ya kigaidi kama vile Boko Haram na Daesh katika maeneo mbalimbali ya nchi.