| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Erdogan na Meloni wajadili kuimarisha ushirikiano wa ulinzi kabla ya mkutano wa NATO jijini Ankara
Rais wa Uturuki amesema nchi yake inalenga kuimarisha ushirikiano na Italia, hususan katika sekta ya ulinzi, kabla ya mkutano wa viongozi wa NATO utakaofanyika nchini jijini Ankara, Uturuki.
Erdogan na Meloni wajadili kuimarisha ushirikiano wa ulinzi kabla ya mkutano wa NATO jijini Ankara
Uturuki kuimarisha ushirikiano na Italia katika nyanja zote, hasa sekta ya ulinzi, alisema Erdogan. / / AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amezungumza kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, ambapo walijadili uhusiano wa mataifa mawili pamoja na masuala ya kikanda na kimataifa.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika siku ya Ijumaa, Erdogan alisema Uturuki inaendelea kuimarisha ushirikiano na Italia katika nyanja zote, hasa sekta ya ulinzi, na kusisitiza umuhimu wa kuchukua hatua mpya za kuendeleza zaidi uhusiano kati ya mataifa hayo mawili, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki kupitia mtandao wa X.

Aidha, Erdogan alisema Uturuki inatarajia mkutano wa viongozi wa NATO utakaofanyika wiki ijayo jijini Ankara utaimarisha mshikamano na umoja wa nchi wanachama wa muungano huo.

Meloni anatarajiwa kushiriki katika mkutano huo.

Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa NATO utafanyika Ankara tarehe 7–8 Julai, ukitarajiwa kuhudhuriwa na viongozi 52 kutoka nchi 32 wanachama wa muungano huo pamoja na nchi tisa zilizoalikwa.

Ushirikiano unaozidi kuimarika

Biashara kati ya Uturuki na Italia ilifikia Dola za Marekani bilioni 32.2 mwaka 2024, hali iliyozifanya nchi hizo kuweka lengo jipya la kufikia Dola bilioni 40 katika mkutano wao uliofanyika mjini Roma mwezi Aprili 2025.

Italia iliendelea kuwa moja ya masoko makubwa ya bidhaa za Uturuki, huku mauzo ya nje ya Uturuki kwenda nchini humo yakifikia kiwango cha rekodi cha dola bilioni 12.4 mwaka 2025.

Ushirikiano katika sekta ya ulinzi pia umeimarika, baada ya kampuni ya Baykar ya Uturuki na kampuni ya Italia Leonardo kuanzisha ubia wa teknolojia za ndege zisizo na rubani mwaka 2025. Aidha, Baykar ilikamilisha ununuzi wa kampuni ya anga ya Italia, Piaggio Aerospace, mwezi Juni mwaka huo.

Italia pia imeendelea kuwa mshirika muhimu wa Uturuki katika sekta ya nishati kupitia Southern Gas Corridor, ambapo bomba la gesi la Trans Adriatic Pipeline (TAP) limekuwa likisafirisha gesi kutoka eneo la Bahari ya Caspian kwenda kusini mwa Italia tangu mwaka 2020.

Kwa sasa, takribani raia 50,000 wa Uturuki wanaishi nchini Italia, huku karibu watalii 740,000 kutoka Italia wakitembelea Uturuki mwaka 2025.

CHANZO:TRT World
Soma zaidi
Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa richa 5 lapiga  mashariki mwa Uturuki
Uturuki inavyopambana kupunguza uvutaji sigara kwa vijana
"Matamshi ya upande mmoja": Uturuki yaikosoa tathmini ya EU kwa kukosa usawa na maono ya kimkakati
Fidan apongeza ziara yake ya Ukraine yenye "mafanikio makubwa"
Uturuki itaendelea na mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la FETO: Erdogan
Julai 15 ilimaliza historia ya mapinduzi ya kijeshi nchini Uturuki: Spika wa Bunge
Erdogan apongeza 'ukaidi wa kishujaa' wa Uturuki ulioshinda jaribio la 'mapinduzi ya kibeberu'
Kutoka mitandao ya kijamii hadi mitaani: Julai 15 na kumbukumbu ya kidijitali ya kiraia ya Uturuki
Julai 15 inaonesha Uturuki haitasalimu amri kwa vikundi vya kigaidi: Waziri wa Mambo ya Nje Fidan
Mke wa rais wa Uturuki Emine Erdogan akumbuka miaka 10 ya jaribio la mapinduzi
Miaka kumi, sauti kumi: Jinsi Julai 15 ilivyobaki katika mioyo ya raia wa Uturuki
Erdogan: Tulidhihirisha uhuru wetu baada ya kushinda jaribio la mapinduzi ya 2016
Uturuki yalaani shambulio la kombora la Wahouthi dhidi ya Saudi Arabia
Jaribio la mapinduzi lililofeli mwaka 2016 liliunda mustakabali wa Uturuki: Burhanettin Duran
Mshikamano uliotibua jaribio la mapinduzi unapaswa kuongoza vizazi vijavyo: Waziri wa Ulinzi
Rais wa Uturuki Erdogan atoa rambirambi jijini Doha kufuatia kifo cha aliyekuwa Emir wa Qatar
Kuunga mkono Uturuki kufuatia jaribio la mapinduzi ilikuwa muhimu : Waziri wa zamani wa Uingereza
Uturuki inataka shule kufuta picha za wanafunzi zilizochapishwa mitandaoni bila idhini ya wazazi
Erdogan: Uturuki itafanya kila iwezavyo kuzuia kutokea tena kwa mauaji ya kimbari kama ya Srebrenica
Uturuki na Misri zatia saini makubaliano ya kuweka msingi wa ushirikiano katika sekta ya ulinzi