| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Abiria wa meli ya MV Hondius kupelekwa Uholanzi baada ya usafiri wa ndege ya Australia kusitishwa
Hii ni baada ya safari ya ndege iliyokuwa imeratibiwa kuwasafirisha abiria hao, kusitishwa.
Abiria wa meli ya MV Hondius kupelekwa Uholanzi baada ya usafiri wa ndege ya Australia kusitishwa
Meli ya MV Hondius./Picha:Wengine

Abiria waliobaki ndani ya meli iliyokumbwa na mlipuko wa virusi vya Hanta sasa watasafirishwa kuelekea Uholanzi badala ya Australia kama ilivyokuwa imepangwa awali.

Hii ni baada ya safari ya ndege iliyokuwa imeratibiwa kuwasafirisha abiria hao, kusitishwa.

Akizungumza katika mji wa Tenerife siku ya Jumatatu, Waziri wa Afya wa Hispania, Monica Garcia alisema kuwa, hapo awali, serikali ya nchi hiyo ilikuwa imeandaa ndege mbili za kuwapeleka abiria hao Australia na Uholanzi.

Hata hivyo, safari ya kwenda Australia haitokuwepo tena baada ya ndege husika kushindwa kuwasili kabla ya muda uliopangwa.

“Hivyo basi, ndege ya Uholanzi itabeba abiria ambao walipaswa kusafiri na ndege ya Australia,” alisema Garcia.

Kulingana na Garcia, watu 54 bado wamo ndani ya meli ya MV Hondius, ambapo 22 kati yao walitakiwa kushuka kutoka kwenye chombo hicho, huku wengine 32, wakibakia ndani ya meli hiyo na kuelekea Uholanzi kwa usafiri wa ndege.

CHANZO:AA