| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Mwanadiplomasia wa Uturuki Fidan ajadili Kupro, Syria na masuala ya kanda na mkuu wa UN Guterres
Katika mazungumzo kwa njia ya simu, pande zote mbili zilijadili kuhusu yanayojiri Mashariki ya Kati na Mashariki mwa Mediterania huku Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa akijiandaa kutembelea kisiwa cha Kupro.
Mwanadiplomasia wa Uturuki Fidan ajadili Kupro, Syria na masuala ya kanda na mkuu wa UN Guterres
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wamejadili masuala ya kanda.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan siku ya Jumapili alijadili masuala yanayojiri katika kanda kwa njia ya simu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Kulingana na vyanzo vya Kidiplomasia vya Uturuki, Fidan na Guterres walijadili yanayojiri katika kanda kwa kuzingatia ziara ya mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa nchini Syria na kisiwa cha Kupro.

Umoja wa Mataifa utawasilisha ripoti kamili kwa Baraza la Umoja wa Mataifa baadaye mwezi huu kuhusu ukiukaji wa Israel nchini Syria, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema siku ya Jumapili.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Damascus, Guterres alisisitiza kuwa ukiukwaji wa uhuru wa Syria “haukubaliki,” akitoa wito kwa Israel kuheshimu Makubaliano ya 1974.

“Kumekuwa na ukatili nchini Syria lakini bado haujawavunja moyo watu wa Syria kuendelea na maazimio yao,” aliongeza.

Alionya kuwa misaada ya Umoja wa Mataifa kwa watu inafikia mahitaji ya karibu asilimia 20 pekee ya watu wa Syria.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliwasili jijini Damascus siku ya Jumamosi kwa ziara ya siku tatu na kufanya mazungumzo na Rais Ahmed al Sharaa na Waziri wa Mambo ya Nje Asaad al Shaibani, wakati ambao alisisitiza dhamira ya Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa Syria, pamoja na mipaka yake na kutoa wito kwa jamiii ya kimataifa kuunga mkono ujenzi mpya wa nchi hiyo.

Umoja wa Mataifa umetangaza siku ya Alhamisi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ataelekea Kupro kupigia chapuo mchakato wa amani.

"Katibu Mkuu atasafiri kwenda Kupro kuanzia Julai 27 hadi Julai 29 kama sehemu ya utendaji wake kazi na dhamira thabiti kwa suala la Kupro," msemaji wake Stephane Dujarric alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Akieleza kuwa Guterres atakutana na Rais wa Taifa la Uturuki la Kupro Kaskazini (TRNC) Tufan Erhurman na Nikos Christodoulides, kiongozi wa Kupro Kusini inayosimamiwa na Ugiriki, Dujarric alisema kuwa mkuu wa Umoja wa Mataifa pia atakutana na "wadau wengine na kujadili juhudi za kuimarisha mchakato wa amani na kuunga mkono usalama katika kisiwa hicho, ikiwemo kutathmini majukumu ya vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa, UNFICYP."

CHANZO:َAA
Soma zaidi
Waziri wa zamani wa ulinzi wa Israel Yaalon amshtumu Netanyahu kwa uchokozi dhidi ya Uturuki
Uturuki itaendelea kuwa chanzo cha matumaini kwa Gaza na dunia: Erdogan
Kenya, Uturuki kushirikiana zaidi katika biashara, uwekezaji na ulinzi
Uturuki yachapisha rasmi sheria ya mchakato wa 'Uturuki Isiyo na Ugaidi'
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki afanya mazungumzo na mawaziri wenzake wa Qatar na Syria
Chombo cha Uturuki cha Marlin chaimarisha uwezo wa kutegesha mabomu baharini
Uwanja wa ndege wa Istanbul waweka rekodi mpya ya ndege na abiria
'Matatizo ya usalama' katika mpaka wa Uturuki na Syria yametoweka: Balozi wa Uturuki
Miaka 25 ya Chama cha AK na kuimarika kwa Uturuki kama mdau muhimu katika kanda na ulimwenguni
Uturuki yataka Tunisia kumuachia kiongozi wa chama cha Ennahda
Austria na Uturuki: Hatua nyingine ya ushirikiano
Uturuki imekamata washukiwa 30 katika operesheni dhidi ya shirika la uhalifu la Alihan Kuris
Erdogan aapa kuipigania dola ya Kipalestina
Rais Erdogan wa Uturuki kukutana na Abbas jijini Ankara kujadili hali ya Palestina
Katika picha: Vivutio mbalimbali vya Uturuki vyang’aa mwanga kushangilia mkataba wa Ulinzi wa Mecca
Rais Erdogan wa Uturuki akutana Kansela Stocker wa Austria
Ndege ya Bayraktar TB2 ya Uturuki yasaidia kudhibiti moto wa nyika nchini Albania
Makubaliano ya Makka ni ya ulinzi wa pamoja lakini hayalengi shabaha au adui yeyote: Waziri Fidan
Uturuki yaadhimisha kumbukumbu ya miaka 59 ya ASEAN na kuahidi kuimarisha ushirikiano wa kikanda.
Uturuki yakanusha madai kuwa Mkataba wa Ulinzi wa Makkah unakinzana na Kifungu cha 5 cha NATO