| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Burkina Faso yafuta takriban asasi 100 za kiraia
Burkina Faso imetoa amri ya kufutwa kwa takriban taasisi na asasi za kiraia 100.
Burkina Faso yafuta takriban asasi 100 za kiraia
Kwa ujumla, taasisi 118, zote zikiwa Burkina Fasa, hivi sasa vimepigwa marufuku kufanya kazi katika nchi hiyo, kwa mujibu wa taarifa ya serikali. / Reuters
16 Aprili 2026

Burkina Faso imetoa amri ya kufutwa kwa takriban taasisi na asasi 100 za kiraia.

Kwa ujumla, taasisi 118, zote zikiwa Burkina Faso, hivi sasa vimepigwa marufuku kufanya kazi katika nchi hiyo, kwa mujibu wa taarifa ya serikali.

Mwezi Julai, 2025, Rais wa mpito Ibrahim Traore alisaini sheria inayozuia makundi ya wanaharakati kufanya kazi, kwa kile kilichoitwa sababu za kiutawala.

Taarifa ya Jumatano iliyotolewa na Waziri wa Tawala za Mikoa Emile Zerbo imewataka wakuu wa mashirika yaliyopigwa marufuku kufuata sheria hiyo ya Julai 2025.

"Yeyote atakayekiuka atakabiliwa na adhabu inayoainishwa katika sheria hiyo," amewatahadharisha.