| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Mamia wajitokeza Afrika Kusini kabla ya hukumu ya kifungo cha mwanasiasa Malema
Serikali inataka Malema ahukumiwe kifungo cha miaka 15 jela, ambaye alipatikana na hatia ya kukiuka sheria za kumiliki silaha mwezi Oktoba.
Mamia wajitokeza Afrika Kusini kabla ya hukumu ya kifungo cha mwanasiasa Malema
Malema alipatikana na hatia ya makosa kadhaa, ikiwemo kumiliki silaha kinyume cha sheria. / Reuters
tokea masaa 2

Mamia ya wanaomuunga mkono kiongozi mtata wa upinzani Julius Malema wakiwa wamevalia nguo nyekundu wamejitokeza katika mji wa Afrika Kusini siku ya Jumatano kabla ya uamuzi wa kifungo chake kwa kufyatua risasi wakati wa mkutano miaka minane iliopita.

Kesi dhidi ya kiongozi huyo wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) iliwasilishwa na shirika la AfriForum, ambalo limefikisha malalamiko yake ya muda mrefu dhidi ya Malema kwa Rais wa Marekani Donald Trump.

Polisi walijitokeza kwa wingi katika mji wa mashariki wa KuGumpo, zamani ukifahamika kama East London, huku wanachama wa EFF wakielekea mahakamani kusikiliza hatua za mwisho za utetezi na kifungo siku ya Alhamisi.

Serikali inataka Malema ahukumiwe kifungo cha miaka 15 jela. Alipatikana na hatia ya kukiuka sheria za kumiliki silaha mwezi Oktoba kwa kufyatua risasi hewani wakati wa mkutano wa sherehe za EFF karibu na mji huo 2018.

Chama cha EFF - ambacho ni kidogo lakini chenye hamasa -kinasema kesi hiyo ni njama za kutaka kumnyamazisha kiongozi huyo mkakamavu, ambaye anafahamika kwa kauli zake kali.

Malema amekuwa akilaumiwa, kwa matamshi yake ya ubaguzi wa rangi akisema, "Wazungu wauawe" – neno ambalo kundi la siasa za mrengo wa kulia linasema ni matamshi ya chuki na ya uchochezi dhidi ya wazungu.

Trump alionesha video ya Malema akitoa matamshi hayo wakati wa mazungumzo yake na Rais Cyril Ramaphosa katika Ikulu ya Marekani mwezi Mei mwaka jana, ambapo kiongozi huyo wa Marekani alisema ni njama mahsusi ya vurugu dhidi ya wakulima wazungu wa Afrika Kusini.

Pamoja na kuwa matamshi hayo ni tata nchini Afrika Kusini, mahakama zimetoa uamuzi kuwa hayana uchochezi na yanatakiwa kuzingatiwa kwa muktadha wa mapambano dhidi ya utawala wa wachache wa wazungu, ambao ulimalizika 1994.

CHANZO:TRT Afrika Swahili