| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Vita vya Iran vyatatiza uchimbaji madini nchini DRC
Waagizaji wa madini ya shaba na kobalti kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamesitisha manunuzi mwezi huu kutokana na kutatizwa kwa usambazaji ambao chanzo chake ni vita vya Iran.
Vita vya Iran vyatatiza uchimbaji madini nchini DRC
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni mzalishaji mkubwa wa madini ya kobalti duniani. / Reuters
tokea masaa 4

Waagizaji wa madini ya shaba na kobalti kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamesitisha manunuzi mwezi huu, kufanya wachimbaji madini kupunguza matarajio yao huku usambazaji kupitia Mashariki ya Kati ukitatizika zaidi, vyanzo vya sekta hiyo vimeiambia Reuters.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndiye mzalishaji mkubwa wa madini ya kobalti duniani na msambazaji mkubwa wa madini ya shaba barani Afrika – kuifanya iwe sehemu muhimu ya usambazaji wa vifaa vya magari yanayotumia umeme na nishati safi.

Baadhi ya wachimbaji tayari wameazna kupata athari. Mzigo wa tani 2,000 ukisitishwa, huku mwingine wa tani 1,800 ukiachwa kuagizwa baada ya mikataba kutiwa saini mapema mwezi Aprili.

Hatari ya uhaba                             

Meli kuchukuwa njia nyingine na kuwepo kwa mizigo michache kumefanya hali kuwa mbaya zaidi, anasema mshauri wa masuala ya madini Isabel Ramirez.

"Kile ambacho kilikuwa kinachukuwa muda wa miezi mitatu sasa kinachukuwa miezi minne, sita," anasema. "Kuna hatari kubwa ya kuwepo kwa uhaba wa bidhaa."

CHANZO:TRT Afrika Swahili